Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 2 August 2015

NI CHELSEA NA ARSENAL LEO KATIKA NGAO YA JAMII

Ligi Kuu ya Uingereza inaanza tena leo Jumapili wakati ambapo mabingwa wa ligi hiyo Chelsea wanakutana na washindi wa Kombe la FA Arsenal katika mechiya Ngao ya Jamii itakayogaragazwa katika uwanja wa Wembley.
Mechi hiyo inajiri siku 64 baada ya kumaliza ligi hiyo na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Aston Villa katika fainali ya FA.
Pende zote mbili hazijafanya usajili mkubwa katika msimu huu ijapokuwa kipa Petr Cech ataanzishwa dhidi ya timu yake ya zamani Chelsea.
Petr Cech
Chelsea vilevile inaweza kumuanzisha mchezaji wao mpya Radamel Falcao.
Falcao mwenye umri wa miaka 29 alihudumu katika kilabu ya Manchester United msimu uliopita lakini hakuweza kutamba kwani aliweza kufunga mabao 4 katika mechi 29 alizocheza pekee.
Siku ya jumapili itazikutanisha timu hizo mbili huku mkufunzi wa Arsenal akitarajia kuishinda timu inayofunzwa na Mourinho kwa mara ya kwanza kati ya mechi 13 walizocheza huku wakufunzi hao wawili tayari wakitofautiana.
Wenger na Mourinho
Mourinho alisema kwamba Arsenal imetumia fedha nyingi msimu huu ikilinganishwa na Chelsea katika kipindi cha miaka kadhaa iliopita ,huku Wenger akijibu kwamba hasikizi kile watu wanachosema ama kufikiri.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment