Pages

Pages

Pages

Wednesday 19 August 2015

KAMATI DRFA YAELEKEZA UCHAGUZI WA TEFA UFANYIKE JUMAPILI HII


Kamati ya uchaguzi DRFA inaelekeza kamati ya uchaguzi ya TEFA kufanya uchaguzi wa viongozi, Jumapili tarehe 23/08/2015 katika ukumbi wa JKT kama ilivyopangwa kufanyika hapo awali.
Kamati pia inapenda  kuutarifu umma kuwa mchakato huu una Baraka zote kutoka TFF, hivyo uingiliaji wowote unakwenda kinyume na ibara ya 6(1)ya kanuni za uchaguzi za TFF 2013 na ibara za 52(6) na 56(6)(a) za katiba ya TFF ambazo zinaelekeza kuwa majukumu ya uchaguzi yapo chini ya kamati ya uchaguzi.
Itakumbukwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jumapili ya tarehe 16,08,2015 uliahirishwa na kamati ya uchaguzi ya Tefa licha ya shirikisho la TFF kuagiza ufanyike,na hivyo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi DRFA wakili Rashid Saadallah akaitaka kamati hiyo ya TEFA kumuandikia barua kueleza sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.
baada ya kupitia sababu hizo,ndipo DRFA ikatoa majibu kwa kuelekeza uchaguzi huo sasa kufanyika jumapili hii.

No comments:

Post a Comment