Pages

Pages

Pages

Saturday 22 August 2015

HUSSEIN BASHE ANENA: UCHAGUZI HUU NI MGUMU

Hussein Bashe

Na Hastin Liumba, Nzega
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa Hussein Bashe amewaambia wanachama wenzake kukaza buti kwani uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu.

Bashe alisema hayo wakati akiongea na wanachama wenzake na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho wilayani Nzega.
Alisema wanaCCM wanatakiwa kutambua kuwa uchaguzi wa mwaka 1995,2000,2005,2010 na huu 2015 kuna tofauti kubwa hivyo wanatakiwa kujipanga.
Alisema uchaguzi utakuwa rahisi zaidi endapo kutakuwa na majibu sahihi ya kero za wananchi zinazowakabili.
“WanaCCM tunapaswa kutambua tuna kazi kubwa kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu…..hapa hakuna kubweteka tunatakiwa kufanya kazi za ziada na kuwaleleza wananchi juu ya kero zinazowakabili.”alisema.
Akizungumzia uhakiki wa wananchi kujiandikisha Bashe alisema hatuwezi kuwa na uchaguzi wakati wananchi watakuwa hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema kujiandikisha na kupiga kura ni haki ya mwananchi hivyo kila mwananchi anapaswa kuhakikiwa ili haki hiyo isipotee.
Aidha alisema kuwepo uchaguzi wakati baadhi ya wananchi hawaoni majina yao wakati walijiandikisha ni kuminya haki hiyo.
Wakati huo huo mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Abrahaman Mdeme alitoa ufafanuzi juu ya mashine za BVR kuendelea kufanya kazi katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo.
Mndeme alisema ni kweli kuna maeneo kuna uhakiki wa majina ya wananchi kama wale ambao picha hazionekani,taarifa zilikosema na uhakiki hufanyika na kupatiwa vingine.
Alisema maneno ya baadhi ya watu kudai uandikishaji huo ni sehemu ya mkakati wa bao la mkono ni uzushi tu.

No comments:

Post a Comment