Pages

Pages

Pages

Saturday 22 August 2015

CHADEMA SIKONGE KWAFUKUTA, MWENYEKITI ADUNDWA KWA 'KUMPITISHA' SAID NKUMBA

Said Nkumba

Na Hastin Liumba, SikongeMWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Lucas Kibelenge amepigwa na wajumbe na wananchi kwa kumtuhumu kukata jina la Mgombea Ubunge Jimbo la Sikonge ambaye alishinda katika kura za maoni.
Kibelenge alipigwa na wajumbe majira ya Saa 4.00 za asubuhi katika maeneo ya nje ya Ofisi ya CHADEMA Wilaya  baada ya kuambiwa asitoke nje ya ofisi hiyo hadi kieleweke kwanini Mgombea aliyepita kura za maoni kukatwa na kumpitisha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Saidi Nkumba ambaye alijiunga hivi karibuni katika chama hicho kutoka CCM.
Mwenyekiti huyo alilazimisha kutoka nje na kuagiza Gari jimuijie hapo baada ya muda gari lilifika na mwenyekiti kuingia ndani kwa ajili ya kuondoka katika eneo hilo, lakini wajumbe walimshusha kutoka kwenye gari na kuanza kumshushia kipigo.
Mgombea aliyechaguliwa na wajumbe no Hija Ranadhani aliyepata kura 83 alikuwa amechakachuliwa Jina lake na kupendekezwa la Saidi Nkumba ambaye hakufanya mchakato wa kura za maoni.
Wajumbe walisema iwapo kama Mgombea wao hata rudishwa Jina lake watachoma moto Ofisi ya chama hicho na Nyumba Nkumba itakuwa hatarini pia.
Kilichosababisha mwenyekiti kupigwa na wajumbe na wananchi ambao walikuwa katika ofisi hiyo no kutoa majibu ya dharau na alisema Kuwa yeye hamuogopi mtu yeyote baada ya kusema hi yo akarusha ngumi kwa mjumbe mmoja ndio wajumbe wengine wakamshushia kipigo cha nguvu.
Kwa upande wa Katibu wa cha hicho Mlagane Katole alisema kuwa mgogoro huo umetokana na baadhi ya mitandao kurusha taarifa kuwa aliyepitishwa kugombea jimbo hilo Kuwait Saidi Nkumba na kuonyesha barua iliyothibishwa kugombea.
Hata hi yo Katibu huyo alisema kuwa na wagomvea watano ambao waliingia kwenye mchakato wa kugombea ubunge jimbo lakini aliyeshinda ni Hijja Ramadhani ambaye alipata kura 83.
Hayo majina yalipelekwa makao makuu ya chama ambayo waliyajadili na kurudisha Jina moja ambalo halijuwepo kwenye mchakato wa kura za maoni ambalo ni la Saidi Nkumba.
Alisema kuwa kurudishwa kwa jina la Saidi Nkumba walishituka na walisikitishwa sana kuona kamati kuu inawasaliti na wamevunja mwongozo wa chama hicho.
Nae Mshauri wa Chama hicho Yusuph Mohamedi alisema Kuwa katika zoezi zima la mchakato la kupata mgombe Nkumba hakuwepo inakuwaje Kamati Kuu Taifa wanarudisha jina hilo .
Mgombea ambaye alipita kura za maoni Hija Ramadhani alisema kuwa yeye alijuwa Mkoani Tabora alipigiwa simu na wajumbe wakamwambia jina lako limechakachuliwa limerudi la Said Nkumba ,wajumbe walimwambia achukuwe usafiri wowote aende Wilaya ya Sikonge watalipa nauli hiyo .
Baada ya muda wa Masaa matatu aliwasili kwa kupokelewa na wajumbe kwa kubebwa juu juu na kumuingiza katika Ofisi ya chama na kudai barua ya kuthibitishwa na kurusiwa kwenda kuchukua fomu na msafara mkubwa ambao waliaompa kura za maoni.
Hijja Ramadhan alipotafutwa alisema atatoa msimamo wake muda wowote kuanzia sasa anahitaji muda kutafakari uamuazi wa CHADEMA taifa.

No comments:

Post a Comment