Bendi maarufu
ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka
FFU-ughaibuni, yenye makao nchini Ujerumani, inatarijiwa kutumbuiza katika
maonyesho makubwa ya muziki na utamaduni Mamling Festival siku ya
jumapili 5 Julai 2015 alhasiri katika viwanja vya Schlosspark, Mamling 3,
Mining nchini Austria. Watayarishaji wa onyesho hilo wameitaja bendi
hiyo ya Ngoma Africa band kuwa muziki wake ni sawa na mzimu unawapeleka
puta washabiki katika maonyesho ya kimataifa na washabiki nchini Austria
wanameisubiria kwa muda wa mwaka mzima. Kikosi kazi hiko chenye tabia
ya kuwatia kiwewe washabiki wake kila waendako na kujizolea washabiki
lukuki kote duniani, kinaupeleka muzimu wa Bongo Dansi nchini Austria. Ziara ya bendi hiyo imeingiliana na mwezi wa Ramadhani wakati baadhi ya
wanamuziki wapo katika swaumu lakini watatekeleza wajibu wao.
Ngoma
Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wake Ebrahim Makunja
almaarufu Kamanda Ras Makunja ni bendi iliyobatizwa majina mengi ya
kiusanii kutoka kwa washabiki majina kama FFU-Ughaibuni, "Watoto wa
Mbwa",Viumbe wa ajabu "Anunnaki Alien' na mengi mengineyo. ni bendi
yenye utajiri ya wanamuziki waliojaa vipaji, na kwa sasa inatamba na
nyimbo zake mbili mpyakatika CD " La Mgambo" za kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda .
Sikiliza at
wasiliana nao at ngoma4u@gmail.com
No comments:
Post a Comment