Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 23 July 2015

MUME WA IRENE UWOYA AIBUKIA STAND UNITED

Mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ akiwa na Irene Uwoya

Na Masoud Masasi
Mwanza. Mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wake kwenye klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya tayari ameshatua mjini Shinyanga kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho na mabosi wa Stand.
Mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo ambao ndio wanaofanikisha mpango huo waliambia gazeti hili kuwa Ndikumana ambaye alikuwa akichezea soka la kulipwa nchini Ubelgiji atasajili kama mchezaji huru kutokana na kumalizika kwa mkataba wake.
Mshambuliaji huyo ameonyesha nia ya kutaka kucheza soka la kulipwa nchini na ndio hasa kwenye klabu hiyo yenye maskani yake mjini Shinyanga.
“Alikuwapo Mwanza na leo amekwenda Shinyanga kumalizana na mabosi wa Stand na mwenyewe anataka kuwaonyesha kazi ameahidi makubwa kama wakikubaliana kwenye usajili wake anataka kucheza soka kwa mara ya kwanza Tanzania, unajua shemeji yetu huyu,” kilieleza chanzo cha habari.
Shabiki mkubwa wa Stand, Fadhili Mlawa aliliambia gazeti hili kuwa ujio wa Ndikumana kutaziba pengo la Abaslim Chidiebele aliyehamia Coastal Union ya Tanga na timu hiyo ilikuwa inahitaji mchezaji mwenye uzoefu wa kuziba pengo hilo. Chanzo kingine cha habari ndani ya Stand kilisema kuwa timu hiyo kwa sasa inahitaji kuongeza washambuliaji wawili wenye uwezo mkubwa ili kuimarisha safu ya ushambuliaji hivyo ujio wa Ndikumana utakuwa umesaidia.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment