Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 5 July 2015

KOMBE LA KAGAME: SIMBA SC YATINGA FAINALI NA BAO MOJA TU!

Kikosi cha Simba SC katika miaka ya 1980.

Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 1981 yalifanyika katika miji ya Nairobi na Kisumu nchini Kenya kati ya Januari 18 na Februari Mosi. Mtandao wa www.brotherdanny.com utakuletea uchambuzi na dondoo mbalimbali za mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 1974.
Jumla ya timu saba zilishiriki mashindano hayo ambazo ni Limble Leaf Wanderers (Malawi), Kabwe Warriors (Zambia) na AFC Leopards (Kenya) ambazo zilikuwa Kundi A. Kundi B lilikuwa na KMKM (Zanzibar), Simba SC (Tanzania), Nile Breweries (Uganda) na Gor Mahia (Kenya).
Mwaka 1981 Simba iliingia fainali na bao 1 na ilimaliza mashindano hayo ikiwa na bao hilo hilo moja.
Katika michuano ya awali Simba SC ilipangwa Kundi B mjini Kisumu, na iliifunga Nile Breweries ya Uganda 1-0 Januari 18, halafu ikatoka suluhu na KMKM ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya.
Gor Mahia yenyewe ilianza kwa kuichapa KMKM mabao 2-0, kipigo ilichokitoa pia kwa Nile Breweries, hivyo ikakusanya pointi 5 na kuongoza kundi hilo. Simba ilishika nafasi ya pili na kufuzu kwa nusu fainali.
Kwenye nusu fainali Simba ilikutana na Limbe Leaf mjini Nairobi Januari 29, ambapo Limbe Leaf ilijipatia bao moja na wakati ikiongoza kwa goli hilo katika dakika ya 86 mlinzi wake akaunawa mpira kwenye eneo la hatari, Simba wakapata penati.
Hata hivyo, wachezaji wa timu hiyo ya Malawi walitoka nje ya uwanja kugomea penati hiyo waliyodai ilikuwa na utata. Jitihada za kuwashawishi warejee kuendelea na mechi zikagonga mwamba.
Hivyo, katika mkutano maalum Cecafa ikaamua kuipa ushindi Simba na kuipeleka katika fainali ambako ilifungwa 1-0 na Gor Mahia. Bao hilo liifungwa na Nashon Oluoch 'Lule'.
Gor Mahia katika nusu fainali ilikuwa imeifunga Kabwe Warriors ya Zambia mabao 2-1 siku hiyo ya Januari 29.
Limbe Leaf Wanderers ilijifariji na nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kabwe Warriors mabao 2-0 Januari 31.
Matokeo kamili ya mechi za mashindano hayo ni haya:

Kundi A
Limble Leaf W. 3-1 Kabwe Warriors
AFC Leopards   0-0 Limble Leaf Wanderers
Kabwe Warriors 3-1 AFC Leopards

 1.Limble Leaf Wd. 2  1  1  0  3- 1  3  [Malawi]
 2.Kabwe Warriors  2  1  0  1  4- 4  2  [Zambia]
 3.AFC Leopards    2  0  1  1  1- 3  1  [Kenya]

Kundi B
KMKM           0-2 Gor Mahia
Simba SC       1-0 Breweries
Gor Mahia      2-0 Breweries  
Simba SC       0-0 KMKM
Gor Mahia      0-0 Simba SC
Breweries      1-0 KMKM

 1.Gor Mahia       3  2  1  0  4- 0  5  [Kenya]
 2.Simba SC        3  1  2  0  1- 0  4  [Tanzania]
 3.Breweries       3  1  0  2  1- 3  2  [Uganda]
 4.KMKM            3  0  1  2  0- 3  1  [Zanzibar]

Nusu fainali
Limble Leaf W. vs Simba SC [Jan 28; Simba ilipewa ushindi wa mabao 2-0; awali ilifungwa bao 1-0 lakini Limbe Leaf Wanderers iligomea penati na hivyo Simba ikapewa ushindi]
Gor Mahia      2-1 Kabwe Warriors

Mshindi wa tatu
Limble Leaf W. 2-0 Kabwe Warriors

Fainali
Gor Mahia      1-0 Simba SC 

KUMBUKUMBU HIZI ZIMEANDALIWA NA MTANDAO WA www.brotherdanny.com. Ukirejea weka chanzo tafadhali cha habari.


No comments:

Post a Comment