Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 1 July 2015

KESI YA ULAWITI YA NTIMIZI KUTAJWA TENA JULAI 6

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Mussa Ntimizi
.
Na Hastin Liumba, TaboraKESI ya kulawiti inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Mussa Ntimizi imezidi kupigwa kalenda baada ya kuahirishwa tena hadi Julai 6 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kukamilika kwa ushahidi.


Kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Tabora inazidi kuahirishwa ikiwa ni mara ya sita sasa baada ya wakili Juma Masanja wa serikali kushindwa kukamilisha mashahidi wa upande wa mashtaka.
Wakili huyo wa serikali aliiomba mahakama kumpa muda wa wiki moja baada ya kumpata shahidi namba tano Dk. Deus Kitapondya aliyetoa ushahidi wake.
Kwa upande wake Dk. Kitapondya anayedaiwa kumfanyia uchunguzi kijana aliyelawitiwa aliiambia mahakama hajapata majibu kutoka maabara hadi sasa hivyo hana uhakika kama kijana huyo alilawitiwa au la.
Alisema kuwa yeye baada ya kumpokea aliyemtaja kama mteja wake ambaye alikuwa hamkumbuki kwa jina wala sura alimpima kama ameambukizwa VVU na magonjwa mengine ya kuambukizwa na kuchukuwa baadhi ya vipimo sehemu ya haja kubwa na kuvipeleka kufanyiwa uchunguzi.
Aidha baada ya ushahidi huo wakili Massanja aliomba kupewa muda wa wiki moja ili kukamilisha ushahidi wake kwa kumfikisha shahidi namba moja ambaye ndiye anayedaiwa kulawitiwa.
Kwa upande wa wakili wa kujitegemea Yusuph Mwangaza Mbili alisema kesi hiyo inaonekana kucheleweshwa kwa kutaka kuahirishwa mara kwa mara kutokana na mshtakiwa kuwa na lengo la kugombea ubunge katika Jimbo la Igalula, wilayani Uyui.
Alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kuthibitisha hilo ni madai yaliyotolewa na mteja wake kuwa  Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Athumani Mfutakamba, aliwaeleza wananchi kuwa kesi hiyo itazidi kupigwa kalenda.
Aliongeza kuwa awali Juni 24 mwaka huu kesi iliposikilizwa mahakamani hapo walimuagiza wakili wa serikali kuwafikisha mahakamani mashahidi wote jambo ambalo limekuwa kinyume na maagizo ya mahakama hiyo hivyo akaomba kupitia kufungu cha Sheria namba 107(a) ambacho kinaipa mahakama nguvu ya kutoa haki ya maamuzi kwa mtuhumiwa.
Aliomba upande wa mashtaka kufunga ushahidi ili mtuhumiwa ajue kama ana kesi ya kujibu ama la ili  apate nafasi ya kufanya kazi zake za kisiasa na kutimiza malengo yake ya kugombea ubunge kupitia chama anachokiongoza.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Jocktan Rushwera amemtaka wakili wa serikali kukamilisha ushahidi ifikapo Julai 6, mwaka huu ili mahakama ikamilishe kazi yake na kumtaka kumpelekea hati ya wito maalumu ya mahakama Mbunge wa Jimbo la Igalula, Athumani Mfutakamba ili kutoa maelezo ya kuingilia uhuru wa mahakama.

No comments:

Post a Comment