Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 3 June 2015

WATANZANIA SABA WATEULIWA KAMATI ZA CAF

Displaying tenga akitoa neno la shukrani.jpg

Rais mstaafu wa TFF na Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Leodegar Tenga, akihutubia wakati wa utoaji wa tuzo kwa wanamichezo mbalimbali. Kulia ni Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi.

Displaying Tenga akipokea cheti kutoka kwa mh. said mtanda.jpg
Rais mstaafu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Chilla Tenga (wa pili kulia) akipokea tuzo yake kutoka kwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Said Mtanda, Mbunge wa Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. Kulia ni Rais wa sasa wa TFF Jamal Emil Malinzi.
Displaying Ndolanga akipokea cheti kutoka kwa mh. said mtanda.jpg
Alhaj Muhidin Ahmad Ndolanga (mwenye baraghashia) akipokea tuzo yake kutoka kwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Said Mtanda, Mbunge wa Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Displaying ggrey mareale na Richard wambura.jpg
Michael Richard Wambura akiwa na Aggrey Marealle (kushoto)

Shirikisho la mpira barani Afrika CAF limewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.

Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:

1. Leodeger Tenga- (Makami Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama).

2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)

3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).

4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)

5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)

6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)

7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
TFF.

Picha za uzinduzi wa jezi mpya zimeambataanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment