Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 2 June 2015

SEPP BLATTER AJIUZULU URAIS FIFA KWA UFISADI

Rais wa FIFA Sepp Blatter
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama rais wa shirikisho hilo kufuatia kashfa ya ufisadi.

Akitangaza kujiuzulu kwak,e Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua rais mpya.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliyopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi.
Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu. 
Shirikisho la FIFA lilikumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na mashtaka ya ufisadi ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliyofunguliwa na Marekani.
Uchunguzi mwengine unaofanywa na serikali ya Switzerland kuhusu vile michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 na 2022 ilitolewa pia unaendelea.
''Nimehusika sana na FIFA na maslahi yake. Kilicho muhimu kwangu ni taasisi ya FIFA na Soka duniani," alisema.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment