Pages

Pages

Pages

Friday 8 May 2015

WADADA WA BONGO MPOOO!? IVORY COAST YAPIGA MARUFUKU MIKOROGO

Wizara ya Afya inasema inadhuru afya ya watumiaji
Ivory Coast imepiga marufuku uigizwaji uuzaji na usambazaji wa bidhaa zozote zenye uwezo wa kuchubua rangi ya ngozi ya binadamu .

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Wizara ya afya imetangaza kuwa ni haramu kuingiza bidhaa hizo katika namna yeyote iwe ni vipodozi ama matembe kwa sababu ya athari zake kwa afya.
Bidhaa nyingi za kijichubua rangi ya ngozi zinauzwa katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Marufuku hiyo inaharamisha uingizwaji wa vipodozi ,mafuta, na tembe zenye madini ya zebaki na vyuma vinavyotumiwa kuchubua rangi pamoja na kemikali zingine nyinginezo.

Mwanamke aliyetumia ''Mkorogo''

Kulingana na afisa wa halmashauri inayosimamia matumizi ya madawa nchini humo Christian Doudouko,
Idadi ya watu ambao sasa wanaonesha dalili za kuathirika kiafya na madawa hayo ya kuchubua ngozi imeongezeka mno katika miaka ya hivi punde na kulazimisha wizara ya afya kuchukua hatua hiyo kali.
Afisa huyo aidha alisema kuwa madini hayo haswa Zebaki yanaweza kusababisha maradhi ya saratani ya ngozi.

Ivory Coast yapiga marufuku ''Mikorogo''

Daktari Elidje Ekra alisema kuwa kemikali zinazotumika ilikuhakikisha ufanisi wa kuchubua rangi asili ya binadamu zinachangia pakubwa kuzuka kwa matatizo ya shinikizo la damu pamoja na hata Kisukari.
Daktari Ekra ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Treichville Abidjan anasema ameshuhudia magonjwa mengi tu ya ngozi yasiyo na tiba na kila alipofanya upelelezi aligundua kuwa wagonjwa walikuwa pia ni watumizi wa mikorogo.
Mikorogo hiyo ya kujichubua ngiozi na maarufu mno katika mataifa mengi ya Afrika huku wanawake wengi wakipendelea kujichubua iliwakubaliwe kuwa ni warembo.

Senegal imeanza kampeini ya kupinga ''mikorogo''

Kasumba hiyo ikichochewa na dhana kuwa mwanamke mrembo sharti awe na ngozi laini na nyeupe.
Matumizi ya mikorogo sasa hata imeanza kupata umaarufu miongoni mwa wanaume.
Licha ya kutokuwepo na takwimu maalum kuhusu matumizi ya mikorogo hiyo, mabango ya mauzo na kunadi bidhaa zenye uwezo wa kukufanya uwe ''Mrembo'' zimezagaa kote barani Afrika.
Haijajulikana hadi sasa wanawake wanaozitumia wamelichukulia vipi kauli hiyo ya serikali.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment