Pages

Pages

Pages

Friday 8 May 2015

TEN-MET YACHOCHEA ONGEZEKO LA WANAFUNZI SHULENI


Na Hastin Liumba, TaboraMTANDAO wa Elimu Tanzania (TEN/MET) umekuwa mkombozi wa elimu nchini baada ya kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto kadhaa ambazo zimekuwa zikikwamisha haki ya elimu.


Akitoa salamu za TEN/MET katika sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Uhamasishaji Elimu kwa wote iliyofanyika kimkoa Mratibu wa Mtandao huo Cathleen Sekwao alisema mtandao huo kwa kushirikiana na serikali na wadau umekuwa mstari wa mbele kuhakikisha suala la elimu linapewa kipaumbele kwa watoto wote.
Alisema tangu kuanzishwa kwa mtandao huo wenye wanachama wapatao 170 sasa  ambao ni mashirika ya kijamii yasiyo ya kiserikali mpaka sasa jitihada zao zimefanikisha ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule sambamba na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi.
Pamoja na kuwepo kwa ongezeko kubwa la uandikishwaji watoto mashuleni Cathleen alieleza siyo watoto wote wanaoandikishwa na kumaliza masomo yao, hivyo akabainisha lengo la TEN/MET kwa mwaka huu ni kuhakikisha jamii inaona tatizo lililopo kwa watoto wa kike kutopelekwa shule au kukatishwa masomo yao.
Alifafanua malengo ya kampeni hii na mchango wa mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ni kuhamasishana, kushirikishana, kushawishiana na kutetea haki ya mtoto kupata elimu bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 Alitaja baadhi ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya elimu hapa nchini kuwa ni pamoja na Sheria na Sera zinazokinzana na haki ya elimu kwa watoto ambazo alizitaja kuwa ni sheria ya ndoa inayomruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri wa miaka 14.
Vikwazo vingine ni mwanafunzi asipokuwepo shuleni kwa siku 90 kufukuzwa shule na mwongozo kwa mtoto wa shule anayepata mimba kutorudishwa shuleni.
Aidha alitaja vikwazo vingine kuwa ni mahudhurio hafifu ya watoto kwa sababu ya kutumikishwa kazi za nyumbani, udhalilishaji wa kijinsia unaofanywa na walimu, ukosefu wa elimu ya haiba na uzazi.
Cathleen alibainisha mbali na Tanzania Education Network/ Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kuchochea ongezeko la wanafunzi mashuleni na kuandikishwa kwa wanafunzi zaidi wenye ulemavu mashuleni pia mtandao huo umehamasisha wazazi kuelewa umuhimu wa elimu kwa watoto.

No comments:

Post a Comment