Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 May 2015

PAC YAHOJI MKUU WA WILAYA KUISHI HOTELI KWA MIEZI MIWILI

Ismail Aden Rage

Na  Goodluck Eliona na Kelvin Matandiko
Dar es Salaam. Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), imebaini madudu katika taarifa za hesabu za mikoa ya Mara na Tanga kwa mwaka 2013/14, zilizowasilishwa kwenye kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini hapa.
Kaimu Mwenyekiti wa PAC, Aden Rage alisema jana kuwa taarifa ya Mkoa wa Mara inaonyesha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Maftah Mohamed amekuwa akiishi hotelini tangu alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete Februari mwaka huu.
“Haingii akilini kumweka Mkuu wa Wilaya hotelini kwa zaidi ya miezi miwili kwa ajili ya kukosa maji, huku ni kumdhalilisha,” alisema Rage.
Rage alisema licha ya taarifa kuonyesha kuwa nyumba ya mkuu wa wilaya imekwishajengwa, lakini bado anaendelea kuishi hoteli, hatua ambayo kamati hiyo imemtaka kuhama hotelini hapo kufikia mwisho wa mwezi huu.
Mjumbe wa kamati hiyo, Gaudence Kayombo ambaye ni Mbunge wa Mbinga Mashariki, ndiye aliyeibua hoja hiyo baada ya kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Benedict Ole Kuyan kueleza kwa nini mkuu wa wilaya huyo bado anaishi hotelini wakati kuna fedha zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya kiongozi huyo.
Kuyan aliieleza kamati kuwa nyumba ya mkuu wa wilaya imekwishakamilika, lakini halmashauri imeshindwa kumkabidhi kutokana na ukosefu wa fedha za kununulia tangi ya maji.
Mhasibu wa Mkoa wa Mara, Merthew Mkumba alisema mkuu huyo wa wilaya amekuwa akikaa katika Hoteli ya Giraffee na kwamba amekuwa akipewa posho ya Sh80, 000 kila siku.
Awali, kabla ya uongozi wa Mara kuhojiwa, PAC ilikutana na viongozi wa Mkoa wa Tanga, huku ikiagiza mambo sita kutekelezwa kutokana na udhaifu uliobainika kutoka maeneo mbalimbali kupitia taarifa hiyo.
Mjumbe wa PAC, ambaye ni Mbunge wa Busanda, Lorensia Bukwimba alihoji Sh24.7 milioni kati ya Sh44 milioni kutumika kinyume na utaratibu uliopangiwa.
Mbunge Mgogoni (CUF), Kombo Hamis Kombo alihoji pia ukiukwaji wa sheria baada ya ofisi za mkoa kuhalalisha matumizi yake kinyume na ilivyopangiwa, huku ikiomba kibali cha kuhalalishiwa matumizi hayo Hazina bila mafanikio.
Kamati hiyo pia ilielezwa kupotea kwa gari la Hospitali ya Mkoa wa Tanga aina ya Land Cruiser bila kutolewa taarifa zozote za maandishi kama sheria inavyoagiza.
Katika majumuisho, Rage aliagiza uongozi huo kuwasilisha barua inayoeleza upotevu wa gari hilo siku Ijumaa wiki ijayo.

Akijibu hoja hizi, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salum Mohamed alikiri baadhi ya udhaifu huku akitoa ufafanuzi wa taarifa nyingine.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment