Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 8 May 2015

MFUTAKAMBA ATAMBA: NIMETEKELEZA ILANI JIMBONI KWANGU

Na Hastin Liumba, UyuiMBUNGE wa jimbo la Igalula wilaya ya Uyui mkoani Tabora Injinia Athuman Mfutakamba amesema anajivunia kazi kubwa aliyofanya kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi jimboni kwake.

Mbunge huyo alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari jimboni kwake.
Moja ya kazi ambayo anajivunia ni kupeleka umeme katika kata za Igalula,Kigwa,Nsololo na Goweko mradi ambao umekamilika mwezi Aprili 30,2015 mradi wenye thamani ya Sh bilioni 4.3.
Aidha alisema umeme mwingine ni wa Kontena (Solar Power) ambao kwa mkoa wa Tabora utatekelezwa wilaya ya Uyui kata zote za jimbo la Igalula.
Kuhusiana na elimu mbunge huyo alisema amesaidia shule kadhaa kwa kutumia fedha zake za mfukoni pamoja na za mfuko wa jimbo ambapo alitoa sh milioni 5.5 shule ya msingi Nsololo.
Alitaja shule nyingine ni Sekondari ya Kizengi sh milioni 5,shule ya Igalula sekondari sh milioni 4,shule ya msingi Vumilia 2.8 na mifuko ya saruji 50 sekondari ya kata ya Goweko na fedha hizo zimetumika kwa ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Katika sekta ya maji mbunge huyo alisema ametumia sh milioni 22,550,000 katika kata za Nsololo, Goweko na kijiji cha Migongwa kwa uchimbaji wa visima virefu na vifupi.
Aidha amesema ametumia kiasi cha sh milioni 57 katika sekta ya afya ikiwa ni kuboresha vituo vya afya na Zahanati zilizoko jimbo la Igalula.
Alisema ametoa vyerehani 2,baiskeli 2 kwa kila kata katika jimbo lake la Igalula kwa vikundi vya kijamii na taasisi za dini ili waweze kujiendesha kwenye vikundi hivyo.
Mbunge huyo amesema hayo ni machache aliyofanya nab ado amekuwa akiendelea kutekeleza ilani ya uchgauzi hado hapo muda wa ubunge utakapokoma.

No comments:

Post a Comment