Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 May 2015

MAJANGA: KANISA LABADILISHWA KUWA MSIKITI

Jumba lililobadilishwa na kuwa msikiti mjini Venice Italia
Iceland imezua hisia kali wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya usanii katika mji wa Venice nchini Italia baada ya kulibadilisha kanisa ambalo lilikuwa halitumiki kuwa msikiti.

Kwa jina 'La Moschea' msikiti huo unatokana na jengo la Santa Maria della Misericordia, kanisa moja la Kikatoliki ambalo lilikodishwa na Iceland na mwenye jengo
Na ili kuonyesha uvumilivu wa kidini waislamu wengi walijitokeza kuomba katika jumba hilo kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wakiwa wamewacha viatu nje ya lango la jumba hilo,waumini hao walielekea Mecca na kusujudu huku wageni wakiendelea na ziara zao za za utalii katika jumba hilo.
Uwekaji wa msikiti huo ulifanywa na msanii mmoja wa Switzerland Christoph Buechel kwa lengo la kuvutia hisia kutokana na kutokuwepo kwa hata msikiti mmoja katika mji wa kihistoria wa Venice--mji ulio na uhusiano wa kihistoria na ulimwengu wa Kiislamu.
Lakini mamlaka ya mji huo imeonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo ikisema kuwa jengo hilo lina hatari ya kushambuliwa na wale wanaopinga Uislamu ama Waislamu wenye itikadi kali.
Rais wa Jimbo la Veneto Luca Zaia ametaja hatua hiyo kama uchochezi.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment