Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 25 May 2015

HALMASHAURI KALIUA YAZINDUA CHF

Na Hastin Liumba, KaliuaHALMASHAURI ya wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora imetakiwa kuhakikisha inafikia malengo ya matumizi ya fedha za uchangiaji mfuko wa afya ya jamii (CHF) katika ununuzi wa dawa zinafikia asilimia 67 toka 20-25.


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kanda ya Magharibi (NHIF) Emmanuel Adina alisema hayo kwenye uzinduzi wa mfuko huo na siku ya wadau wa CHF wilayani Kaliua.

Siku hiyo ya wadau ilishirikisha madiwani wote,watendaji wa kata na vijiji,viongozi wa dini,makundi maalumu ya watu,wajumbe wa kamati za afya na mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi Profesa Juma Kapuya.

Adina alisema viongozi wote wanatakiwa kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa na njia pekee ni kuhamasisha wananchi kwenye vikao vya maamuzi.

Aidha alishauri vyombo vyote vya uwakilishi wa wananchi ikiwemo bodi ya halmashauri ya huduma za matibabu na kamati za afya za vituo zinakutana mara kwa mara na kupanga namna ya kupata maoni.

Adina aliwaomba washiriki kwenye uzinduzi huo kutumia fursa za mikopo za vifaa tiba kwa vituo vya matibabu kwa kuwa na vifaa vya kisasa vya uchunguzi.

‘Suala la wananchi kuhamasishwa kujiunga na CHF lisiachiwe kwa idara ya afya pekee bali ni ajenda ya kudumu kwenye vikao vyenu vya maamuzi.’alisema Adina.

Aliomba wadau wote washirikishwe kutoa maoni kwa lengo la kujenga hasa kupeendekeza michango,kiwango ambacho kitakidhi mahitaji ya upatikanaji wa huduma bora.

No comments:

Post a Comment