Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 May 2015

HAILE GEBRESELASSIE ASTAAFU RIADHA

Nguli wa mbio Haile Gebrselassie akifurahia ushindi.
Haile Gebrselassie ametamka bayana kustaafu mbio za ushindani. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 42 mwenye asili ya nchi ya Ethiopia amethibitisha uamuzi wake wa kustaafu ufukuzaji upepo, na hii ni mara baada ya kuhitimisha mbio za 16 za Great Manchester mapema leo Jumapili.

Uamuzi huo unahitimisha safari ya miaka 25 ya ufukuzaji upepo safari ambayo iliwahi kumpatia medali mbili za dhahabu za michuano ya Olympiki, ushindi mara nane wa dunia wa riadha na kuweka rekodi duniani ya kufanya vyema mara 27 katika mbio ndefu duniani.
Mwenyewe Haile Gebrselassie anasema; "Nastaafu mbio za ushindani, sio kustaafu kukimbia! Huwezi kuacha kukimbia, mbio ni maisha yangu." Haile ameyasema hayo nguli huyo wa ufukuzaji upepo alipokuwa akifanya mahojiano na shirika la BBC kitengo cha michezo.
Gebrselassie anabakia kuwa mkimbiaji mwenye rekodi ya kipekee tena mashuhuri katika mbio za meta 2,000 duniani alizozimaliza kwa muda wa saa moja.
Suala la kutaka kustaafu riadha alilisema miaka mitano iliyopita na ni baada ya kupata ajali michezoni lakini akarejea katika mbio miezi kadhaa baadaye.
Gebrselassie alishindwa kuonesha uwezo wake adhim kabisa katika mbio za London za Olympiki mwaka 2012 lakini si haba alishinda mbio za The Great Scottish huko Glasgow mwaka mmoja baadaye, na akaendelea kusumbua katika mbio za Vienna City katika  mbio za nusu marathon.
Sasa baada ya kung’ara katika mbio za ushindani za mwishoni mwa wiki mjini Manchester mbio ambazo amekuwa kinara wa ushindi kwa miaka mitano mfululizo na kumaliza mbio ambazo amekuwa akizifurahia mara zote.
"Ninayo furaha kusita hapa ama kuachia hapa, nilikuwa najua fika kuwa hii ni mara yangu ya mwisho kuufukuza upepo," amesema nguli huyo wa mbio za Marathon anayetambulika fika katika ulimwengu wa michezo na dunia kwa ujumla.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment