Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 4 April 2015

WAKULIMA TUMBAKU KATAENI KUDHULUMIWA -RC


Na Hastin Liumba, Tabora
WAKULIMA wa zao la tumbaku mkoani Tabora wameaswa kukataa kila aina ya dhuluma zinazofaywa na taasisi au watu binafsi wakiwemo baadhi ya wanunuzi wa zao hilo ili kuondokana na dimbwi la umaskini linalowakabili.



Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini SuleimanKumchaya alitoa wito huo kwa niabayaMkuu wa mkoa wa Tabora LudovickMwananzila mkutano wa 22 wa ChamaKikuu cha Ushirika wa Wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi (WETCU) mjini Tabora.

Alisema kwa jinsi ya kawaida mapato ya fedha za kigeni zinazotokana na mauzo ya tumbaku kama mkulima angekuwa anazipata zote kama zilivyo asingekuwa na hali alinayo sasa, lakini sasa hali ni tofauti kwani viongozi wao wakati mwingine huwaingiza katika mikataba isiyoeleweka.

“Alibainisha wapo watu wachache wanaojinufaisha kiujanjaujana kutokana na zao hilo, kupitia mikataba mibovu na utitiri wa madeni…..ndio maana mkulima ambaye ndiye mzalishaji mkuu anapouza mavuno yake hapati kiasi alichouza,” alisema.

Ni vizuri mkulima akaomba mkopo wa pembejeo, nyumba bora au ushirika ukaomba mkopo wa kununua lori kwa ajili ya shughuli za chama haya ni ya kimaendeleo zaidi, ni aibu mkulima kuomba mkopo wa kununua kuni za kukaushia tumbaku.

Aidha alishauri mikopo wanayokopa irejeshwe kwa uaminifu na kufanya biashara endelevu huku akishauri wawe makini na wanunuzi wa vichochoroni kwani hawatambuliki kisheria.

Naagiza bodi ya WETCU na vyombo vingine vya serikali hususani Maofisa Ushirika wa halmashauri zote kukataa kila aina ya dhuluma anayofanyiwa mkulima wa tumbaku.

Katika hili la utoroshaji tumbaku na wizi unaofanywa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu katika vyama vya wakulima Kumchaya aliagiza TAKUKURU, RPC na Ma OCD kushirikiana na WETCU ili kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa.

Awali Mwenyekiti wa WETCU Mkandala Gabriel Mkandala alisema uongozi mzuri, uaminifu na uadilifu ndio kioo cha maendeleo akawataka watendaji wote wa vyama hivyo kubadilika kwani baadhi yao ndio wanaokwamisha maendeleo ya wakulima kwa kuendekeza tamaa ya fedha na kuingia mikataba isiyoeleweka.

No comments:

Post a Comment