Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 4 April 2015

VINYOZI FC YAWANYOA UVCCM TABORA 2-0


Na Hastin Liumba, TaboraTIMU ya Vinyozi wa nywele ya kata ya Kiloleni Manispaa ya Tabora imetawazwa  bingwa wa mashindano ya ‘Kapipi Cup’ baada ya kuichapa timu ya vijana wa UVCCM Kiloleni.



Kufuatia ushindi wa mabao 2-0 timu hiyo  imefanikiwa kunyakua zawadi ya mbuzi dume na kitita cha fedha taslimu sh 100,000.

Mchezo huo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Kiloleni hiyo ulikuwa na shamrashamra za kipekee na timu zote zilionyesha kandanda safi na ya kuvutia jambo lililowafanya mashabiki lukuki waliofurika kushuhudia burudani ya aina yake.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Emanuel Mwakasaka alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza timu ya Vinyozi FC walikabidhiwa fedha taslimu sh 100,000 na mbuzi wakati mshindi wa pili timu ya UVCCM walikabidhiwa fedha taslimu sh 100,000.

Mwakasaka ambaye ni mdau mkubwa wa michezo katika mkoa huo aliwaasa vijana kujibidisha zaidi katika michezo ili kuinua vipaji vyao kwani michezo inatoa ajira nzuri  kwa vijana walio wengi na kwa wale wasiopenda michezo aliwataka kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupata mikopo itakayosaidia kuboresha maisha yao.

Awali Mwandaaji wa mashindano hayo Juma Kapipi ambaye ni mtangazaji wa kituo cha runinga cha ITV alieleza kuwa mashindano hayo yaliyoanza kutimua vumbi tangu tarehe 12 Machi hadi 28 Machi mwaka huu yalilenga kuwaweka vijana pamoja na kuinua vipaji vyao kupitia michezo na kuwahamasisha wajiepushe na vitendo vinavyoathiri nguvu kazi yao.

Alisema mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 8 zilizoko katika kata hiyo licha ya kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa yamekuwa na mvuto mkubwa kwa vijana walioko katika kata hiyo na kata zote za Manispaa ya Tabora.

Timu zilizoshiriki mashindano hayo ni Gola FC, Bodaboda Kilolelni, Bodaboda Stendi, Mafundi Selemala, Kiloleni Star, Majimaji, UVCCM na Vinyozi.

No comments:

Post a Comment