Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 11 April 2015

TWIGA STARS YAFUZU FAINALI ZA AFRIKA


MSHAMU NGOJWIKE NA FARAJA MASINDE, DAR ES SALAAMTIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, jana ilifuzu kwa mbinde fainali za Michezo ya Afrika ‘All African Games’ baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Zambia ‘Shepolopolo’.

Licha ya kipigo hicho, Twiga Stars imenufaika na ushindi wa mabao 4-2 iliyoupata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka, Zambia na hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 6-5.
Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Congo, Brazzaville Septemba mwaka huu.
Bao la kuongoza la Twiga Stars lilifungwa na Asha Rashid dakika ya pili ya mchezo baada ya kuunganisha vema pasi ya Anastas Katunzi na kuwachanganya mabeki wa Zambia na kupiga shuti lililojaa moja kwa moja wavuni.
Timu hizo zilishambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 12, Mwanahamisi Sharua alikosa bao la wazi, baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya lango la wapinzani wao.
Chisa Rachel wa Shepolopolo alikosa bao dakika ya 16 baada ya kufanya shambulizi kali na shuti lake kutoka nje ya lango la Twiga Stars.
Dakika ya 29, Mwanahamisi Shurua aliandika bao la pili kwa Twiga Stars akiungusha pasi safi ya Asha aliyefunga bao la kuongoza.
Kipindi cha pili kilianza kwa Shepolopolo kufanya shambulizi kali na kupata bao dakika ya 50 kupitia kwa Grace Chanda aliyeunganisha krosi ya Barbra Banda.
Twiga Stars ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Donisia Daniel na Anastas na nafasi zao kuchukuliwa na Fatuma Salum na Etoe Mlenzi, huku Shepolopolo wakimtoa Annie Kibanjo na kumuingiza Ireen Lungu.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwa Shepolopolo ambapo dakika ya 60 walipata bao la pili kwa mkwaju wa penalti iliyowekwa wavuni na Barbra, baada ya Grace Chanda kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Shipolopolo ambao walibadilika kipindi cha pili na kucheza soka la uhakika, waliongeza bao la tatu na ushindi dakika ya 90 kupitia kwa Misozi Chisa aliyepiga shuti lililomshinda kipa wa Twiga Stars na kutinga wavuni.
Twiga Stars: Fatuma Omar, Anastas Katunzi, Stumai Abdalla, Fatuma Makusanya, Fatuma Issa, Sophia Mwasikili, Donisia Daniel, Amina Ally, Sherider Boniface, Asha Rashid na Mwanahamisi Sharua.
Shepolopolo: Hazel Natasha Nali, Rachel Nachula, Lweendo Chisamu, Joana Benai, Mary Mwakapila, Mary Mwilomba, Misozi Chisa Rachel, Meya Banda, Annie Kibanjo, Grace Chanda na Babra Banda.

CREDIT: MTANZANIA

No comments:

Post a Comment