Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 12 April 2015

TASWIRA YA VURUGU ZILIZOTOKEA IRINGA JANA

Askari  wa FFU wakiwa katika msako  wa  kuwasaka  waliohusika na  vurugu hizo eneo la Ipogolo  mjini Iringa. (CREDIT: MATUKIODAIMA)
Moshi wa  bomu la machozi  ukiwa angani
Moshi  ukiwa  umetanda  angani
Bomo  la machozi  likilipuka  angani 
Askari  wa zimamoto  wakizima moto katikati ya  barabara  ya  Iringa – Kilolo  leo
Askari  wa zimamoto  wakifungua  barabara
Askari  wa FFU  wakiwa kazini
Askari  wa Zimamoto akitoa  taili  lililokuwa  likiwaka barabarani
Wananchi  waliokuwa  msibani  wakishuhudia msako  mkali wa  polisi
Barabara  ikiwa  imefungwa
Askari  wa jeshi la  Zimamoto na  uokoaji mjini Iringa  akisaidia kumvusha  mzee  ambae  alikuwa akikimbia mabomu na  kujificha mtaroni
Mzee  huyo  akimpongeza  askari kwa  wema  wake
Baadhi ya  watuhumiwa wa  vurugu hizo  wakipakiwa katika gari la  FFU
Magari ya  polisi  yakisafirisha  watuhumiwa wa vurugu kwenda  kituo  cha polisi kati
Wananchi  wakiwa katika  vurugu  hizo  huku baadhi yao  wakishuhudia
Mpita njia  eneo la Ipogolo akipiga  picha kwa simu moto  uliokuwa  ukiwaka barabarani
 Na  MatukiodaimaBLOG
 
VURUGU kubwa  zilitokea jana katika  eneo la Ipogolo  mjini Iringa na kusababisha askari wa   kikosi cha kutuliza  ghasia  (FFU)  kutumia mabomu ya machozi  kuthibiti vurugu baada ya mtoto wa  miaka kata 6 kugongwa na gari  wakati  akifanya biashara ya  kuuza mbogo mboga.

Wananchi wanaosadikika  kuwa na  hasira kali  walianza kuwashambulia
askari  polisi waliofika kuchukua mwili huo kwa mawe  kwa madai ya
kuchelewa  kufika  eneo la  tukio.
 
Wakizungumzia tukio hilo kwa mwandishi wa habari hizi  baadhi ya  wananchi walisema  kuwa  mtoto   huyo  aligongwa  majira ya saa 7 mchana na zaidi ya saa  moja baada ya  kutoa taarifa  polisi  ndipo  walipofika  eneo la  tukio jambo lililowakwaza  wananchi hao.
 
Walisema kuwa  mbali ya  polisi  hao  kufika  pia tayari  baadhi ya askari waliopo eneo hilo la stendi kuu ya Ipogolo  kwa  kushirikiana na wananchi  walifanikiwa  kulikamata  gari  ambalo  lilisababisha ajali hiyo.
 
Alisema Neema Sanga  kuwa wakati  tukio  la kugongwa  mtoto  huyo  likitokea alikuwa jirani na eneo hilo katika  msiba  na kuwa  wakati  akiwa ameingia ndani ya nyumba  hiyo  yenye msiba  kusaidia  kugawa  chakula ghafla  alipata taarifa  kuwa wananchi  wameanza vurugu kwa  kuchoma moto mataili katika barabara  hiyo  kuu ya  Iringa- Kilolo.
 
Hata hivyo  alisema  kuwa  tukio  hilo  lilichukua  zaidi ya dakika 45 polisi  hao wa FFU  kufika na kuanza  kutuliza  vurugu  hizo kwa  kupiga mabomu ya machozi  kuwatawanya  wananchi zaidi ya 500  waliokuwa wamekusanyika eneo hilo kuzuia  magari  kuendelea kupita katika barabara  hiyo  huku  baadhi yao  wakitaka  kufunga  barabara  kuu ya Mbeya  – Iringa ambayo haihusiki ka bisa na   eneo  lililotokea  tukio
hilo.
 
"Ni  kweli  mtoto kagongwa na gari na kufa  tukio ambalo ni kusikitisha sana na  polisi baada ya  kupigiwa simu  wamefika  eneo la  tukio na kuchukua maiti ya  mtoto  huyo lakini  tunajiuliza kwanini  vijana hao kuanza  kuwapiga mawe  polisi na kufanya  vurugu  wakati gari lililogonga mtoto huyo  likiwa  limekamatwa ..”  alihoji Bi Sanga.
 
 Kuwa kwa  upande  wake hakuona  sababu za  polisi  kupigwa  wala  wananchi hao kuchoma moto  barabara wakati ajali  hiyo kama ajali nyingine na tayari  gari  lililosababisha ajali  likiwa  limekamatwa.
 
Bi Sanga  alisema  wakati  mwingine  polisi  wanalalamikiwa kuwa wanatumia  nguvu  zaidi  ila kwa  tukio  hilo lawama  zake anazipeleka
kwa  wananchi wenzake ambao walionyesha  kufanya vurugu kwa kuchomo moto  barabara  hiyo ya lami na   kupiga  polisi huku  wakitambua  wazi polisi si  waliosababisha ajali  hiyo.
 
Huku kwa  upande  wake mmoja  John Kalinga  akiomba  serikali kupitia
wizara ya miundo  mbinu  kuangalia uwezekano  wa  kuweka matuta katika
eneo hilo kwa madai kuwa  hii ni ajali ya pili kutokea na kusababisha vifo  toka  eneo hilo  lilipowekwa  lami.
 
Mwandishi wa habari hizi  alishuhudia baadhi ya  vijana wakikimbilia kujificha katika nyumba  moja  iliyopo eneo hilo ambayo ilikuwa na msiba huku baadhi yao  wakijifungia  katika maduka na bar zilizopo eneo hilo kabla ya  polisi  kuwafuata na  kuwakamata huko walikojificha na kuwaacha wale waliokimbilia msibani.
 
Kamanda wa  polisi  wa  mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi hakuweza  kupatikana kuzungumzia tukio  hilo  huku idadi ya vijana  waliokamatwa  kwa tuhuma za  kuhusika katika  vurugu  hizo zaidi ya 20  walionekana  wakipagiwa katika magari  ya  polisi.

No comments:

Post a Comment