Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 4 April 2015

SERIKALI KUDHIBITI UTOROSHAJI TUMBAKU


Na Hastin Liumba,TaboraSERIKALI mkoani Tabora imesema itahakikisha inawadhibiti wakulima wanaotosha tumbaku na kusababisha vyama vya ushirika vya msingi kuingia kwenye madeni makubwa.


Mkuu wa mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila alisema hayo wakati akifunga mkutano wa 22 wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi (WETCU).

Mwananzila alisema madeni mengi yaliyopo sasa yanasabishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi na wakulima wenye tamaa kutokuwa waadilifu hivyo serikali itakula sahani moja nao.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kama serikali na wadau wa zao hili tusipokomesha uchafu huu tutaua ushirika wetu.

Aidha alisema bado kuna utaratibu mbovu kwenye malipo ya wakulima kwani upo mtindo wa wakubwa kulipana kwanza ndipo wakulima walipwe hali asingependa kuiona inaendelea.

Alisema serikali pia imejipanga vyema kuhakikisha inadhibiti baadhi ya viongozi wa vyama kuingia mikataba ya siri na hatima yake wakulima wanakuja kubebeshwa mzigo mzito wa madeni.

Alisema viongozi wa namna hiyo serikali itahakikisha wanang`olewa mapema ili wasiwaingize wakulima kwenye madeni na kuwasababishia umasikini.

Hata hivyo alionya baadhi ya wakulima wa tumbaku kuacha tabia ya kuweka uchafu kwenye tumbaku ili kuongeza kilo za tumbaku na akaonya atakayebainika hatua zitachukuliwa dhidi yake.

Alisema vitendo hivyo vitashusha hadi ya tumbaku ya Tanzania na alisihi usimamizi uwepo eneo hilo na serikali itasimamia zoezi hilo.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku kanda ya magharibi (WETCU) Mkandala Mkandala alisema kwa upande wao watahakikisha maagizo ya serikali yanatekelezwa.

Mkandala alisisitiza vyama vyote kuweka uzalendo mbele na kuwa waadilifu ili wajikomboe hapo walipo na kuondokana na umasikini.

No comments:

Post a Comment