Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 16 April 2015

MIAKA 30 JELA KULAWITI MWANAFUNZI


NA Hastin Liumba,TaboraMAHAKAMA  ya wilaya ya Tabora imemhukumu  Masudi Nassor  (20) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti mwanafunzi wa kike wa shule ya msingi mwenye umri wa miaka tisa.


Akitoa hukumu hiyo leo hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Bahati Chitepo alisema kwamba ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia hiyo.

Alisema kwamba kitendo alichofanya kijana huyo mwenye nguvu ya kufanya kazi na kupata mwenzi wake ambaye alinalingana naye umri inaonesha wazi alifanya hiyo makusudi.

Hata hivyo hakimu Chitepo alisema ushahidi kuliotolewa mbele ya mahakama hiyo kutoka kwa mganga aliyemuhudumia mtoto huyo katika hospitali ya kitete inaonyesha wazi  mshitakiwa alimwingilia mtoto huyo kinyume na  maumbile yake na kumsababaishia maumivu makali.

kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mwendesha mashitaka wa serikali aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwani mshitakiwa huyo ni kosa lake la pili hivyo adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya.

Awali mwandesha mashitaka wa serikali aliambaia mhakama hiyo kwamba mnamo januari 22 mwaka huu majira ya asubuhi katika kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora masudi Nassor anaendesha baskeli alikutana na mlalamikiwa akiwa anakwenda  shuleni na kuombwa lifti .

Baada ya kupandisha kwenye baiskele Masudi alikwenda naye kwenye pori la Kalunde ambapo alimlawiti mara tatu na kumtelekeza huko kisha kukimbia lakini alikamatwa na askari jeshi aliyekuwa dori katika kambi hiyo na kumfikisha polisi.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo aliiomba mhakama hiyo impunguzie adhabu kwani anaishi na babu yake mlemavu wa mguu na wazazi wake wote walishafariki dunia.

No comments:

Post a Comment