Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 16 April 2015

MAYWEATHER KULINDA MENO KWA DOLA ELFU 25, AFANYA MAZOEZI HADHARANI

Kifaa cha kulinda meno chenye thamani ya dola za kimarekani dola elfu ishirini na tano,kitahusika kulinda meno ya bondia Floyd Mayweather

Taarifa kutoka jarida la Forbes la nchini Marekani zinasema Mayweather atatumia kifaa cha kulinda meno (mouth Guard) chenye gharama ya dola za kimarekani elfu ishirini na tano.

Katika hatua nyingine, na katika hali isiyotarajiwa bondia raia wa Marekani Floyd Mayweather ameamua kufanya mazoezi ya wazi na kuruhusu vyombo vya habari kuchukua picha ikiwa ni maandalizi kuelekea katika pambano lake dhidi ya bondia Manny Pacquiao raia wa Philippine.
Floyd Mayweather akifanya mazoezi mtaani na kuruhusu apigwe picha.
Mayweather ambaye ni bingwa wa WBA na WBC, ameweka rekodi ya kucheza mapambano 47 ya kulipwa bila kupoteza hata moja wakati mpinzani wake amepigana mapambano 57, akiwa amepigwa mara tano na kutoka sare mara mbili.
Pambano kati ya wawili hao linatarajiwa kufanyika mnamo May 2 mwaka huu, huku pigano hilo likitajwa kuwa ndio la pesa nyingi zaidi katika historia ya ngumi duniani.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment