Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 15 March 2015

WANAWAKE MSIWE NA WIVU, HAMTABARIKIWA

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
ARUSHA: IMEELEZWA kuwa pamoja na kuwa baadhi ya wanawake wanadai kuwa wameokoka na wanampenda Mungu lakini bado hawatekelezei sheria na tabia ya Mungu ambayo ni upendo badala yake wengi wao wanasumbuliwa na tabia ya wivu.
 
Hataivyo tabia hiyo ya wivu wakati mwingine inasababisha wengi wao kumosea Mungu huku chanzo cha wivu vikiwa ni vitu vidogo vidogo sana. 
Mchungaji Japhet Nanyaro wa kanisa la T A G Patmo Nkoanekoli ndiye aliyeyasema hayo katika semina ya kina mama ya neno lamungu ambayo iliwakutanisha kwa pamoja wanawake. 
Japhet alisema kuwa kwa sasa wanawake wengi sana wanakabiliwa na suala zima la wivuy hasa pale wanapoona mwenzao ameinuka kwa kiwango Fulani jambo ambalo wakati mwingine linawaweka katika mpango wa shetani bila ya wao kujua huku wakidai kuwa wameokoka. 
Aliongeza kuwa yeyote yule ambaye nadai kuwa anaishi maishaya mazuri ya Kimungu ni lazima ndani yake awe na upendo kwani Mungu ni upendo na kama hauna Upendo basi wewe sio wa Mungu. 
Wakati huo huo alitaja madhara ya wivu ambao upo kwenye baadhi ya mioyo ya kina mama kuwa ni pamoja na kutembea na chuki  jambo ambalo nalo halipendezi kabisa mbele za Mungu. 
“Tunapaswa kuhakikisha kuwa tunaishi maisha ya kupendana na vinyongo havijengi bali huwa vinabomoa kila mara hata kama mwenzako amepata  kuliko wewe usimchukie"aliongeza mchungaji huyo.
Pia alisema kuwa ili kudumisha zaidi upendo kunatakiwa kuwa wawazi hasa kwa wale ambao wametukosea ambapo maandiko yanasema kuwa tusilale na vinyongo kwani wakati mwingine vinyongo havisaidiii hata kidogo bali vinabomoa.

No comments:

Post a Comment