Pages

Pages

Pages

Thursday 11 December 2014

SINGIDA INA ZIATA YA TANI 520,370 ZA CHAKULA

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Alli akimkabidhi zawadi ya mzinga wa nyuki mkazi wa wilaya hiyo, Benton Nollo ili kuendeleza ufugaji wa nyuki kwa vijana. Alli amekuwa akisaidia vijana wanaoonyesha juhudi katika ufugaji wa nyuki na kuku. Picha na Habel Chidawali 
Na Gasper Andrew, Mwananchi
Singida. Mkoa wa Singida umefanikiwa kuvuna mazao ya chakula tani 913,143 katika msimu wa 2013/2014, hivyo kuwa na ziada ya chakula ya tani 520,370.
Hayo yalisemwa juzi na katibu tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan alipokuwa akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa malengo ya kilimo kwa msimu wa 2013/14 na malengo ya kilimo kwa msimu wa 2014/15 mbele ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).
Alisema msimu uliopita, mkoa ulijiwekea lengo la kulima hekta 554,227 za mazao ya chakula, na kwamba zilizolimwa ni hekta 540,739 ambazo ni sawa na asilimia 96.
Alifafanua kuwa katika hekta hizo wamefanikiwa kuvuna tani 913,143 wakati mahitaji halisi ya chakula kwa wakazi 1,434,411 wa mkoa huu ni tani 392,773.
Kwa upande wa mazao ya biashara, Liana alisema jumla ya tani 363,922 zilivunwa baada ya kulimwa hekta 226,162 sawa na asilimia 93 ya lengo la kulima hekta 243,419.
“Kwa jumla hali ya uzalishaji ni nzuri ikionyesha wastani wa uzalishaji wa mazao ya chakula kuwa asilimia 117 na asilimia 99 kwa mazao ya biashara,” alisema katibu tawala huyo wa mkoa.
Aidha, alisema msimu wa 2014/2015, mkoa umejiwekea lengo la kulima hekta 553,165 za mazao ya chakula zinazotarajiwa kuzalisha tani 959,836.87 na hekta 312,506.45 za mazao ya biashara zinazotarajiwa kuzalisha tani 433,770.07.
Awali, akifungua kikao hicho, mkuu wa mkoa, Dk Parseko Kone aliwapongeza wakulima kwa juhudi waliyoionyesha. “Napenda kuwahimiza viongozi kuendelea kutoa elimu ya kutunza chakula na kutumia kilichopatikana kwa uangalifu,” alisema Dk Kone. Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha kuwa mvua za mwanzo zilizoanza kunyesha ni za kupandia na kutaka wahusika kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima mapema.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment