Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 1 December 2014

MAVAZI YA WATOTO WA OBAMA YAKOSOLEWA, WAAMBIWA VAENI MKIWA BAA!

Rais Barack Obama akiwa na watoto wake Sasha na Malia

Sasha na Malia
Watoto wa rais wa Marekani Barrack Obama,Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa Shukran.

Elizabeth Lauten ,ambaye ni mkurugunzi wa mawasiliano wa mbunge Stephen Fincher alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo baadaye yalifutwa.
Baada ya kukosolewa Bi Lauten aliomba msamaha kwa kutoa matamshi hayo ya kukera.
Alikua akikosoa skati fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.
Bi Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.
Maandishi yake yalisoma:''Kwa wapendwa Sasha na Malia:najua kwamba bado muko katika usichana wenu lakini ninyi ni miongoni mwa familia ya kwanza ya taifa hili, tafadhali jaribuni kuwa na heshima.Tafadhalini jaribu kuheshimu jukumu mulilopewa.
''Mama yenu na baba yenu hawaheshimu nyadhfa zao kama inavyohitajika na taifa kwa jumla.
"Kwa hivyo naona kwamba mnakosa ile hadhi ya kuwa kioo cha jamii. Maandishi hayo yaliendelea na kuwashauri wasichana hao kuonyesha kwamba wanaishi katika Ikulu ya White House.
Vaeni mavazi ya kuonyesha mnahitaji kuheshimiwa sio kama mko katika baa."
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment