Pages

Pages

Pages

Thursday 11 December 2014

KAFULILA: NITAKOMAA NA SETHI MPAKA KIELEWEKE

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila, akiwahutubia wananchi katika mji mdogo wa Nguruka, wilaya ya Uvinza, mkoani Kigoma juzi.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, (pichani)  amesema yupo tayari kupambana hadi mwisho na mtendaji mkuu wa IPTL na PAP, Harbinder Singh Sethi, ili kutetea maslahi ya Watanzania kufuatia uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow.


Akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Nguruka katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma juzi baada ya kumpokea katika maandamano makubwa, Kafulila alisema yupo tayari kupambana na Sethi licha ya vitisho anavyopata toka kwa watu mbalimbali.

“Juzi nimemsikia anasema anatafakari upya kuangalia uwezekano wa kuendelea kuwekeza nchini, eti atang’oa mitambo yake aipeleke sehemu nyingine…nazidi kumwambia nitapambana naye licha ya kulindwa na Ikulu,” alisema Kafulila.

Aidha, Kafulila aliwataka wananchi wa jimbo lake kutochangia ujenzi wa maabara zinazojengwa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete, mpaka hatua zitakapochukuliwa dhidi ya waliohusika na ulaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema moja ya chama kinachounda Ukawa, Jessica Kishoe, aliwataka wananchi kutokichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa serikali za mitaa, badala yake wawachague viongozi watakaokuwa na uwezo wa kuinyooshea kidole serikali ya CCM.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment