Pages

Pages

Pages

Sunday 2 November 2014

VIGOGO SABA RELWE WAWEKWA KIKAANGONI

Waziri wa Uchukuzi,Dk Harrison Mwakyembe.PICHA|MAKTABA 
Na Suzan Mwillo, Mwananchi
Dar es Salaam. Hatima ya viongozi watano wa ngazi za juu wa Mamlaka ya Reli nchini (TRL) kung’olewa au kubaki madarakani, itajulikana ndani ya siku saba baada Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuunda kamati ya uchunguzi wa matatizo ndani ya TRL.
Viongozi hao walio kikaangoni ni Mkurugenzi wa TRL, Amani Kisamfu, Kaimu Mkurugenzi Pascal Mafikiri, Ofisa Rasilimali Watu, Pius Kaberehe, Ofisa Mawasiliano aliyetajwa kwa jina moja la Nduezabura na mhandisi aliyetajwa kwa jina mmoja la Masai.
Sanjari na hilo, hatima ya malalamiko ya nyongeza ya mshahara na malimbikizo ya fedha kwa wafanyakazi hao itajulikana ndani ya kipindi hicho.
Hatua hizo zimefikiwa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kutembelea wafanyakazi hao jana na kuzungumza nao juu ya changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi, kufuatia madai ya wafanyakazi hao kutaka kugoma kwa kipindi cha wiki moja.
Baada ya Dk Mwakyembe kuwasili ofisi za TRL mchana, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Erasto Kihwele alieleza kuwa viongozi hao wamekuwa mizigo na kwamba ndiyo wanaowakwamisha katika utekelezaji wa majukumu. Kihwele, alizungumzia pia suala la nyongeza ya mshahara na kumwomba Dk Mwakyembe kulipatia ufumbuzi haraka.
Malalamiko hayo ndiyo yaliyomlazimu Dk Mwakyembe kuunda kamati ya watu watatu ili kufanya uchunguzi wa kina, kabla ya kuwachukulia hatua stahiki viongozi hao.
“Siwezi kuwahukumu hawa kabla ya kuchunguza kwanza juu ya hizo tuhuma. Hivyo, nitafanya kazi na hiyo kamati, ndani ya wiki moja tutakuja na majibu ya matatizo yenu yote. Lazima tuwajibishane,”alisisitiza Dk Mwakyembe.
CREDIT: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment