Pages

Pages

Pages

Friday 7 November 2014

UHARIBIFU WA MISITU YA AMAZON KULETA JANGA BRAZIL

Msitu wa Amazon
Mtaalamu wa masuala ya hali ya hewa ameiambia BBC kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya uharibifu wa mazingira katika msitu wa Amazon na mfululizo wa ukame nchini Brazil.

Sao Paulo
Takwimu zinaonye kuwa ukame huo umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo.
Dr. Antonio Nobre ambaye ni mtaalamu wa hali ya hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa.
Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari.
Serikali nchini humo iansema imelazimika kuanzisha mgao wa umeme kutokana na uhaba wa maji ikiwa ni moja ya hatua za dharula.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment