Pages

Pages

Pages

Friday 7 November 2014

UBELGIJI WAANDAMANA KUPINGA SERA YA KUONGEZEWA MUDA WA KUSTAAFU

Waandamanaji Belgium
Polisi nchini Ubelgiji katika mji mkuu Brussels, Ubelgiji wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na maji ili kuwatawanya waandamanaji wanaopinga sera ya kutaka kuongeza muda kustaafu kwa watumishi wa umma pamoja na kupunguza bajeti ya huduma za jamii.

Waandamaji hao ambao pia walikuwa wakiwasha moto, wameunguza magari,wamerusha mawe na uharibifu mwingine.
Serikali ya umoja wa kitaifa ya Ubelgiji inasisitiza kuwa mabadiliko yanahitajika na kwamba mabadiliko hayo yanapaswa kupunguza tofauti ya mahitaji ya bajeti ili kuendana na miongozo ya jumuiya ya Ulaya.
Machafuko nchini humo yalianza mwezi marchi mwaka huu pale waandamanaji kwa mara ya kwanza walioingia mitaani wakiwa na mabango yanayopinga baadhi ya sera nchini humo.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment