TAASISI ya Starkey Hearing Foundatioin ikitoa huduma ya kliniki kwa kuwawekea vifaa vya kuongeza usikivu masikioni kwa watu zaidi ya 1000 wenye matatizo ya kusikia katika Mkoa wa Kilimanjaro shughuli iliyoanza jana kwenye viwanja vya Shree Hindu Mandal vilivyopo kando ya barabara ya Mawenzi mjini Moshi . Pichani, mwanzilishi wa taasisi hiyo, Bill Austin na mkewe Tani wamekuwa wakiongoza zoezi hilo toka lilipoanza majira ya saa mbili asubuhimjini Moshi jana.

Lina John ambaye ni kipofu akipima kiwango cha sauti kwenye kidevu chake ili kama mtoto Ronald anaweza kusikia mara baada ya kuwekewa kifaa cha kuongeza usikivu:
Wasichana ambao ni marafiki Lina John ambaye ni albino pamoja na Esther Urassa kutoka Shule Maalumya Mtakatifu Francis iliyopo katika Manispaa ya Moshi walikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wanatoa msaadakwa watu waliokuwa wanapewa huduma ya kuwekewa vifaa maalum.
CREDIT: FULLSHANGWE BLOG



No comments:
Post a Comment