Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Juma Nkamia.
Na Muhibu Said, Dodoma
Hatimaye serikali imetangaza rasmi kwamba, itawasilisha bungeni muswada wa sheria ya habari, Februari, mwakani.
Hatua hiyo inatokana na sheria ya sasa ya habari kulalamikiwa muda mrefu na wadau wa habari kuwa ina upungufu mkubwa wa uhuru wa habari na vyombo vya habari.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (pichani), alisema jana kuwa taratibu zote za kupeleka muswada huo bungeni zimekamilika.
Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Seleman Bungara, jana.
"Taratibu zote za kuleta muswada wa sheria hiyo zimekamilika na Mungu akijalia inshaallah muswada huo utaletwa mwezi wa pili mwakani," alisema Nkamia. Katika swali lake la nyongeza, Bungara ambaye ni maarufu kama "Bwege", alisema ni siku nyingi wadau wa habari, vikiwamo vyombo vya habari na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa wakitaka muswada huo wa sheria upelekwe bungeni.
Hata hivyo, alisema mpaka leo muswada huo haujafika bungeni ili sheria itakayotungwa kutokana na muswada huo, itoe ukandamizaji katika sheria iliyopo hivi sasa.
"Je, ni lini serikali itaileta sheria hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?" alihoji Bungara kabla ya swali lake hilo kujibiwa na Nkamia.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment