Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 17 November 2014

MKUTANO MKUU WA ACT KUFANYIKA NOVEMBA 20, 2014


Na Abdallah Khamis, Dar es Salaam
CHAMA Cha Alliance for Change and Transparance, (ACT-Tanzania), kinatarajia kufanya mkutano mkuu maalum wa Taifa wa chama hicho  Novemba 20 mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa muda wa ACT-Tanzania Samson Mwigamba wakati akiwapokea wanachama wa vyama mbali mbali waliojiunga na chama hicho.
Mwigamba alisema mkutano mkuu umelenga kupitisha katiba ya chama hicho itakayowapeleka katika uchaguzi wa viongozi watakaoongoza kwa muda wa miaka mitano kwa mujibu wa katiba hiyo.
Akitoa kadi kwa wanachama wapya waliojiunga nao, Mwigamba alisema chama hicho hakiwezi kuchagua ni wanachama wa chama gani ajiunge kwao, bali kinawataka watanzania wote kujiunga kwa kuwa milango ipo wazi.
Miongoni mwa waliojiunga hiyo jana ni pamoja na Tony Kamukanda, aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika jimbo la Korogwe mjini mwaka 2010.
Wengine ni  Ramadhan Hamis, aliyewahi kuwa kaimu mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (Cuf) wilaya ya Ilala na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gongo la Mboto.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment