Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 7 November 2014

MAJUU HAMNAZO: JAMAA AEGESHA NDEGE NJE YA BAA NA KWENDA KUPIGA ULABU!


Majuu kweli hamnazo! Mwanamume mmoja wa Australia ameshtakiwa na polisi baada ya kuegesha ndege nje ya baa na kuingia ndani kupiga ulabu.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa ndiyo kwanza ameinunua ndege hiyo ndogo isiyo na mabawa aina ya Beechcraft inayoweza kupakia watu wawili tu na wakati akirejea nyumbani akaamua kusimama kwenye baa ili apate moja-moto-moja-baridi.
Aliishusha ndege hiyo kwenye lami katika mtaa mkubwa huko Newman, Western Australia, na kisha kuiegesha ndege hiyo nje ya Hoteli ya Newman, huku akiiacha injini ikiunguruma.
Polisi walisema jamaa alipopimwa kuona kama alikuwa amelewa (breathalyser test) aliweza kufaulu pengine kwa kuwa ndiyo kwanza alikuwa amegida bia ya kwanza, lakini akashtakiwa kwa kuhatarisha maisha, afya na usalama wa wakazi wa eneo hilo kwa sababu pangaboi lilikuwa bado linaendelea kuzunguka.
Wakazi wa eneo hilo walishangazwa kuona ndege ikiwa ikiwa imeegeshwa nje ya hoteli maarufu mtaani hapo.
"Nikiwa ninarejea kutoka mjini... ghafla nikashangaa kuona ndege imeegeshwa nje ya Purple Pub," Beau Woolcock alikiambia kituo cha radio cha ABC.
"Kitu kingine cha kushangaza ni kuona polisi wa eneo hili akiwa anachungulia kwenye mlango wa ndege kana kwamba alikuwa anaulizia leseni ya rubani."
Mhudumu wa baa kwenye Hotali ya Newman alisema jamaa alikuwa kijana wa mjini ambaye aliwazuga viongozi wa baa kwa 'kujifanya bubu' wakati alipohojiwa na polisi.
Lakini Sajini Mark McKenzie wa Polisi hapo Newman alisema: "Watoto walikuwa wanarejea kutoka shule. Hali ingeweza kuwa baya.
"Watu wanadhani kwamba kilikuwa ni kichekesho, lakini ilikuwa hatari sana na hatujafurahishwa na kitendo hicho."

CREDIT: BROTHERDANNY BLOG NA MASHIRIKA

No comments:

Post a Comment