Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana
(kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) baada ya kupokewa na
mamia ya wananchi jimboni humo kufanya ziara ya kuimarisha chama wilayani humo.
Kinana na msafara wake alitembelea miradi ya mbalimbali ya maendeleo pamoja na
kuzungumza na wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana
akilima shamba kwa kutumia treka katika shamba la ufuta lililopo katika Kijiji
cha Mkotokuyana, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, pembeni yake ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias
Chikawe maybe alikuwa anashuhudia tukio hilo la ulimaji. Kulia ni Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Kinana alitembelea miradi mbalimbali ya
maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wilayani humo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (katikati
aliyevaa kofia) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe wakati alipokuwa
anajibu maswali ya wananchi wa Kijiji cha Mkotokuyana wilayani Nachingwea.
Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Kinana alitembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wilayani humo.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana
akizungumza na wananchi wa mjini Nachingwea kuhusu maendeleo yaliyopatikana katika
Jimbo hilo pamoja na changamoto mbalimbali zinazozikabili jimbo hilo. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe ambaye aliitwa kwa ajili ya kuwafafanulia masuala
mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya tangu alipoanza kuliongoza jimbo hilo.
Mamia ya wananchi waliudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini
Nachingwea.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya
wananchi wa jimbo hilo baada ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulhaman Kinana
(hayupo pichani) kumpa nafasi ya kuzungumza na wananchi wake. Chikawe alisema
tangu alipoanza kuliongoza jimbo hilo mwaka 2005, shule za sekondari zilikuwa
tatu na mpaka sasa zipo 26. Pia jimbo lake sasa halina shida ya maji baada ya
kuzinduliwa mradi mkubwa wa maji jimboni humo. Kinana pamoja na msafara wake
wapo mkoani Lindi katika ziara ya kuimarisha chama pamoja na kutembelea miradi
mbalimbali maendeleo. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment