Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 1 November 2014

JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM MKOA WA DAR YAZINDUA DAFTARI LA WANACHAMA WAKE

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Daftari la wanachama wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Anautoglo. Anayeshuhudia kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje. 
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed (kushoto) na Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje wakionesha daftari hilo baada ya kuzinduliwa.

 Viongozi wa meza kuu wakipiga makofi wakati wakiimba wimbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuzindua daftari hilo. Kutoka kulia ni Katibu Msaidizi wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Mavela, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu,Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje ,  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed, Katibu wa Elimu na Malezi Taifa, Masoud Bwire na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Dar es Salaam, Nicolaus Msemo.
 Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Katibu wa Jumuia hiyo mkoa wa Dar es Salaam, Ali Cholaje (kushoto), akiteta jamba na wajumbe wa kamati ndogondogo zilizoundwa ili kurahisisha utendaji kazi wa jumuia hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Wilaya ya Ilala,Meritius Mangugu na Angelina Malembeka.
 Wajumbe wa Kamati ya Afya, Maafa na Mangira wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Ali Said, Josephat Kadiya na Dk. Meshack Sabaya.

 Wajumbe  wakijadiliana jambo, Kutoka kushoto ni Omar Njate, Seleman Kumchaya na Seleman Nduda.
Wajumbe wa Kamati ya Uhamasishaji, Mapambo na Makazi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Janeth Sondoka, Amina Mlewa na Khadija Kingi.
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wajumbe wa Kamati ya Elimu na Malezi wakifurahia jambo. Kutoka kulia ni Amina Mtemvu, Levocatus Machage, Maria Ernesti na Galila Ramadhan.
Wajumbe wakiwa katika uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale


 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Seif Shaban Mohamed amewata viongozi wa jumuia hiyo kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuifanya jumuia hiyo kukua kiuchumi.



Mwoto huo aliutoa wakati akizindua Daftari la Wanachama wa Jumuia hiyo Mkoa wa Dar es Salaam leo.



"Nawapongezeni kwa kuunda kamati ndogondogo ndani ya jumuia itasaidia kusogeza huduma kwa wanachama wetu na wananchi kwa ujumla hivyo kukifanya chama chetu kiendelee kuaminiwa" alisema Mohamed.



Alisema tunarasimali kubwa ni vizuri sasa tukazitumia rasimali hizo kukuza uchumi wa jumuia yetu na msipende kusubiri kila kitu muelekezwe na viiongozi wa juu.


No comments:

Post a Comment