Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 18 November 2014

HIZI NDIZO REKODI ZA KUSHANGAZA ZA EDWARD LOWASSA

Kapteni Lowassa akipiga tizi mjini Dodoma

Na Emma Kaaya via Wanabidii

Edward Lowassa ndiye Waziri Mkuu aliyewai kukaa katika kiti cha uwaziri mkuu kwa muda mfupi zaidi kuliko waziri mkuu yeyote yule; sasa angalia hii rekodi yake ya kushangaza:

Mosi,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha nia ya dhati kukabiliana na foleni ya jiji la Dar, tatizo ambalo kimsingi ni kama jinamizi kwa sasa!!!!

Mbili,
Ndani ya muda mfupi sana alionyesha kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana. Pale bandarini kulikuwa na watu waliokuwa vibarua kwa muda wa zaidi ya miaka 15 lakini alipoingia uwaziri mkuu, ile hali kaisimamia mpaka  jamaa wale wakapata mikataba ya kudumu.

Tatu,
Ndani ya muda mfupi alionyesha kujali elimu kwa wananchi. Hizi shule za kata ambazo ndizo zinazosaidia wananchi kuamka kwa sasa ni matunda ya Lowassa.

Nne,
Tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Akiwa bungeni mara nyingi amekuwa akiongelea suala hili la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kiasi kwamba ilibaki kidogo tu ingekuwa malalamiko ya mikopo kwa wanafunzi yangekuwa historia.

Tano,
Wakati akiwa waziri mkuu, kwa muda mfupi sana ilionekana kuwa uchumi sasa utapaa; na tayari kulikuwa na viashiria (indicators) vya kutosha katika hilo.

Sita,
Kwa muda mfupi sana utendaji serikalini ulikuwa unakwenda kwa kasi ya ajabu. Kuanzia mdogo hadi mkubwa.

Saba,
Kwa muda aliokaa hajawahi hata mara moja kutoa kauli tata za kuashiria ubabe kwa wale wanaopingana naye. Kauli zake siku zote zimekuwa very straight kuwakabili watumishi wazembe na watendaji wanaotenda kazi katika mfumo wa business as usual. Tazama alivyomwajibisha Mhandisi wa Manispaa ya Temeke mara baada ya ghorofa la Chang'ombe Village lilipoporomoka; Tazama alipoamua kuingilia katika mkataba wenye utata wa kampuni ya maji Dar, hakusubiri siasa zichukue nafasi, tofauti na sasa.

Nane,
Ndiye kiongozi pekee serikalini ambaye ana rekodi ya kutoa individual support kwa mwananchi mmoja mmoja pale atakapobaini kuwa panahitajika support kwa ajili ya huyo mwananchi. Hata BBC Swahili walishawahi kuripoti kuhusu hili.

Tisa,
Akiwa waziri mkuu alimbeba sana Kikwete kwenye utendaji wa kiserikali! Hadi sasa Kikwete amekata tamaa kabisa na mambo ya serikali. Anatamani siku anarudi toka Maryland akute tayari 2015 imefika maana hana hamu kabisa na mwenendo wa mambo ndani ta taifa hili.

Kumi,
Kikwete hatakaa amsahau kwa kumpoteza katika utendaji wa serikali yake. Na ndiyo maana uchaguzi wa 2010 Kikwete alipata shida sana! Na hadi leo anamlilia sana, ila mfumo wa chama chake unamgandamiza sana.

HAYA SASA
Kuna waliokaa kwa muda mrefu ambao waliishia kuwaambia wafanyabiashara "...Ukitaka mambo yako yawe mazuri jiunge na CCM...!"

CREDIT: Kwa hisani ya Wanabidii ingawa imehaririwa na Moderator.

No comments:

Post a Comment