Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 3 October 2014

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KUWEKEZA KWENYE SHULE YA WAZAZI LEGURUKI


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog

MERU: WADAU wa elimu hapa nchini wameombwa kuwekeza katika shule ya jumuiya ya wazaziLEGURUKI iliopo Meru mkoani Arusha kwani bado ina uwezo wa kutoa elimu kwa wanafunzi wengi ingawaje kwa sasa wapo wachache sana.

Hayo yalielezwa na mjumbe wa siasa ya mkoa wa Arusha ambaye pia ni kiongozi katika jumuiya hiyo ya wazazi,John Palangyo wakati akiongea na gazeti hili kuhusiana na miradi mbalimbali ambayo ipo chini ya jumuiya hiyo.


Palangyo alidai kuwa shule hiyo ya wazazi Leguruki ina uwezo mkubwa sana wa kutoa kwa wanafunzi zaidi ya 400 lakini kwa sasa wanafunzi ambao wapo ni kama 100 pekee jambo ambalo linasababisha hasara kubwa sana ya uendeshaji wa shule hiyo.

Alidai kuwa kilichosababisha shule hiyo kuyumba ni baada ya baadhi ya walimu pamoja na viongozi wa shule kuingiza siasa hali ambayo ilifanya idadi ya wanafunzi izidi kupungua siku hadi siku

“kwa kweli shule yetu ina uwezo mkubwa sana wa kusaidia kuongeza na kuimarisha elimu kama wadau lakini hata wazazi na walezi wataweza kujumuika na kisha kuwekeza tena kwenye shule yetu hii kwani hata baadhi yavyombo vya habari vinasema kuwa wapo wanafunzi wanaoshindwa kupata elimu bora kwa kuwa hawana madarasa  lakini kwa sisi hapa kwetu tunayo tena ya kutosha;”aliongeza palangyo.

Alidai kuwa mpaka sasa tayari wameshaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuboresha mazingira ya shule hiyo lakini pia kufanya shule hiyo iwe miongoni mwa shule ambazo zinawafaulisha wanafunzi  hasa kwenye mithiani ya kitaifa

Naye Katibu wa jumuiya hiyo Daniel Mgaya alisema kuwa tayari wakaguzi wa ndani wameshakagua mahesabu na mali mbalimbali za shule hiyo ambazo zilitumika vibaya na kusababisha madeni makubwa hivyo wahusika watachukuliwa hatua kali ikiwemo kushitakiwa ili iwe fundisho kwenye jamii.

Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Loi alisema kuwa pamoja na kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini bado elimu inayotolewa shuleni hapo ni nzuri na hivyo wazazi, walezi wanatakiwa kuendelea kuitumia kwa ajili ya maslahi ya umma.

No comments:

Post a Comment