Pages

Pages

Pages

Wednesday 1 October 2014

JACK MUGENDI ZOKA ATEULIWA KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA

Jack Mugendi Zoka

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.

IMETOLEWA NA
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam,
Septemba 30, 2014

No comments:

Post a Comment