Ndugu
zangu,
Tunapoelekea
kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 lazima tutafakari ni Rais gani ambaye
atatufaa. Kwa maoni yangu, tunahitaji Rais anayewapa majukumu watendaji wake na
kusimamia utekelezaji. Ambaye yuko tayari kuwajibika na kuwawajibisha watendaji wake pindi wanaposhindwa
kuwajibika wenyewe.
Tanzania ili iendelee inahitaji Kiongozi
shupavu kweli kweli asiye na masihara. Taifa lipo kwenye umaskini mkubwa, watu
wanateseka bila sababu ya msingi.
Tunahitaji Rais Shupavu, Jasiri,
Mthubutu, Mwenye kuweka malengo na kusimamia utekelezaji wake ili tuyafikie
hayo ‘Matokeo Makubwa Sasa’ katika maeneo yote muhimu kuanzia kwenye elimu,
uchumi, kilimo, ulinzi na usalama, na zaidi kurudisha uzalendo kwa wananchi.
Tunahitaji Rais anayeweka
vipaumbele na kutambua namna tunavyoweza kufikia, siyo kwa kujaza makaratasi
kwenye makabati.
Tunahitaji Rais asiyeyumba,
ambaye upepo ukipuliza anapoteza mwelekeo. Lazima ahakikishe anakabiliana na
mawimbi kwa manufaa ya umma.
Tunahitaji Rais ambaye ni dikteta
kidogo na mwanadiplomasia kidogo ili mambo yaende. Mtu anayeweza kuchukua hatua
mara moja mambo yanapokwenda kombo badala ya kusitasita.
Tunahitaji Rais msikilizahi,
mfuatiliaji, asiye kigeugeu wala mvivu.
Tunahitaji
viongozi ambao wanafuatilia utendaji, wanafanyia kazi taarifa na changamoto za
wananchi na taifa kwa ujumla. Wanaoweza kuchukua hatua mapema kabla mambo
hayajaharibika.
Tena basi
hata watendaji wake wanapaswa kuwa wanamipango wenyewe badala ya kusubiri Rais
awapangie.
Hakika,
zama za 'kula bata' kwa mawaziri kwa kutumia kodi za walalahoi ziishe sasa
kabla hatujaingia mwaka 2015, vinginevyo tutaanza kuwawajibisha hata mawaziri
na wabunge mara watakapokuja kuomba kura zetu.
Hakuna
binadamu aliyekamilika, lakini kwa hotuba hii - haijalishi Kiingereza chake kibovu
kwa sababu siyo lugha yake ya asili - hakika Jenerali Iddi Amini hakuwa mbaya
kiasi hicho, alikuwa dikteta lakini alipenda uwajibikaji na matokeo bora.
Mnasema jamaa hakuwa msomi, kwa hotuba hii naamini huhitaji kuwa na lundo la
shahada ndipo utambue kwamba Iddi Amini alikuwa anajali uwajibikaji kwa maslahi
ya wananchi wote - siyo uzembe na kufumbiana macho!
Kwa hiyo,
wale ambao wanaota ama kuoteshwa kugombea urais mwaka 2015, wangeoteshwa pia
kama wano uwezo wa kuthubutu kufanya kama Jenerali Iddi Amini - kidikteta
kidogo na kidemokrasia kidogo - kinyume chake taifa litazama!
Haya ni
maoni yangu tu.
Ndugu
yenu,
Daniel Mbega
0656-331974
No comments:
Post a Comment