Pages

Pages

Pages

Monday 1 September 2014

WATAKIWA KUWATHAMINI NDEGE ILI WAONGEZEKE

Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: WANANCHI wanaoishi  Kijiji cha Ngaresero kwenye eneo la Ramsar la Ziwa Natron, Wilayani Ngorongoro, wametakiwa kuthamini ndege waliopo eneo hilo, ili wazidi kuzaliana na kuvutia watalii.
Wito huo umetolewa jana na Meneja wa Eneo  hilo, Mihindi Baso, wakati alipokuwa kwenye sherehe za maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ndege wahamao Duniani, zilizofanyika kijiji cha Ngaresero, kwenye eneo la Ramsar la Ziwa Natron, ambazo ziliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ndege, “Birdlife International”.
Alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuhimiza wananchi watunze mazingira ya ndege hao, ili wasije kuhama na kwenda kutafuta eneo lingine la kuzaliana.
“Ndege hawa huhama kila mwaka, lakini wanaenda hadi Ulaya na kurudi Tanzania kwenye eneo hilo ili kuzaa watoto wao, jambo ambalo ni sifa na linavuta sana utalii,”alisema.
Aidha alisema wao kama ofisi wameamua kufungua ofisi eneo hilo li kuwa karibu na wananchi na kutoa elimu juu ya utunzaji wa ndege hao, wawe kivuti cha watalii hata vizazi vijavyo.
Alisema ni wazi ndege hao hufika eneo hilo sababu ya amani na asilimia 75 hadi 80 ya ndege hao wanazaliwa Natron, jambo ambalo ni sifa kubwa Duniani.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kutunza hata ndge wengine siyo Flamingo tu, ili ikiwezekana nao waje kufanya makao ya kuzaliana hapo.
Naye Sweetbart Lwelushengo, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alisema ndege hao wamechangia kuzipatia familia za eneo hilo kipato, kutokana na utalii wa wageni wanaofika kijijini hapo.
Alisema kuwa hata wao kama serikali wanakaribisha hata wawekezaji waje eneo hilo kuwekeza na wtawekewa mazingira mazuri, ili mradi ndege hao wapate mazingira salama ya kuzaliana kwao.
Alisema hadi kufikia sasa wageni zaidi ya bilioni moja hufika Wilayani humo na kupita eneo hilo kwa ajili ya kuangalia ndege hao wa ajabu ambao wanahama kila mwaka na kurudi eneo hilo kwa ajili ya kuzaliana.

No comments:

Post a Comment