Pages

Pages

Pages

Monday 1 September 2014

WANAHABARI 50 KUTOKA ARUSHA KUNUFAIKA NA MRADI WA MIAKA MITATU


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha: SHIRIKA la msaada wa sheria hapa nchini (NOLA)linatrajia kutoa mafunzo ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu kwa wana habari zaidi ya 50 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa malengo ya kusaidia jamii kuweza kupambana na biashara hiyo haramu.
Pia mafunzo hayo yataweza kuwasaidia waaandishi hao kuandika vema habari hizo ingawaje kwa sasa bado waaandishi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Akizungumza na Brother Danny Blog mara baada ya kufungua mafunzo yaliyowashirikisha wana habari wa mkoa wa Arusha, mratibu wa mradi wa kupmbana na usafirishaji haramu wa binadamu Doto Mwelo alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 hapa nchini.
Mwelo alidai kuwa wanahabri zaidi ya 50 kwa upande wa mkoa wa Arusha wataweza kunufaika na mafunzo hayo lakini pia vitu muhimu ambavyo vitaweza kuwasaidia kufanya kazi hiyo kwa urahisi sana.
“Huu mradi ni wa miaka mitatu na kwa sasa ndio tumeanza kutoa mafunzo kwa baadhi ya wanahabari hapa nchini tunatarajia kuwa baada ya miaka mitatu kukamilika basi wataweza kusaidia jamii kuepukana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu”aliongeza Mwelo.
Wakati huo huo alidai kuwa pia mara baada ya kumalizika kwa mradi huo watabuni njia nyingine ya kuweza kuwasaidia waaandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi na kwa maslahi ya hali ya juu.
Awali mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo ambayo yaliwajumuisha wanadishi wa habari utoka mkoa wa Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela alisema kuwa Fani ya habari ni moja ya fani ambazo ni muhimu sana katika maendeleo ya nchi na ni lazima jamii iweze kuwapa kipaumbele kwani inachangia sana mabadiliko kwenye sekta zote.
“Kwa mfano siku moja waandishi wa habari wakagoma kuandika basi nina amini kuwa siku hiyo nchi haitakuwa na furaha hata kidogo kila mtu atajikuta akiwa na wasiwasi mkubwa sana  sasa huo ni mfano mdogo tu napenda kuwaambia kuwa waandishi wa habari ni muhimu kwa maendeleo yetu” aliongeza Mongela.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha(APC)Claud Gwandu alisema kuwa kupitia mradi huo wa miaka mitatu mkoa wa Arusha utapata mabadiliko makubwa sana hasa katika masuala ya biashara haramu ya binadamu na hivyo ni jukumu la wadau wengine nao kuweza kuunga mkono jitiada hizo.

No comments:

Post a Comment