Pages

Pages

Pages

Thursday 4 September 2014

WACHUNGAJI WASHAURIWA KUTOTAMANI MALI ZA WAUMINI WAO ILI WASIWAVUNJE IMANI ZAO


Na Mwandishi Wetu, Brother Danny Blog

Arusha:
VIONGOZI wa dini mbalimbali hapa nchini wameshauriwa kuhakikisha kuwa kamwe hwaingiliwi na roho ya tamaa dhidi ya mali za waumini wao na kisha kuanza kutoa maandiko ili wapatiwe mali kwani hali hiyo inasababisha asilimia kubwa ya waumini wa Kikristo kushuka viwango vya imani.
Aidha kitu kikubwa sana ambacho kinasababisha viongozi hao waweze kupatwa na tamaa ni kwa kuwa wanaona baadhi ya waumini wao wanamali za kifahari sasa mali hizo wakati mwingine zinasababisha waweze kupata tamaa ya kuwa nazo.
Hayo yameelezwa na Mchungaji Anthony Jokakuu wa Kanisa la EAGT Moria wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo lilolopo maeneo ya Mbauda mapema wiki hii katika semina iliyowashirikisha waumini pamoja na wananchi mbalimbali waishio pembezoni mwa kanisa hilo.
Mchungaji Anthony alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya waumini ambao wamebarikiwa kuwa na mali au magari ya kifahari kuliko wachungaji wao sasa kutokana na hali hiyo wapo baadhi ya wachungaji ambao wanatumia vyeo vyao kwa hila na tamaa na kisha kuwaambia waumini kuwa wanatakiwa kuanza kujitolea vityu vya kifahari.
Alisema kuwa mara wanapowaambia waumini wao waweze kujitolea vitu vya kifahari wakati mwingine wanalazimika hata kutoa uongo mkubwa unaoendana na kiblilia  ili waweze kupata kile ambaco wanakitaka  na wakishakipata basi wanaingia mitini bila kujua kuwa hali hiyo inaweza kuchangia sana kumrudisha nyuma mkristo ambaye anamungalia mchungaji kama baba yake wa kiroho.
“Tamaa za mali za waumini kamwe hazipzawi kupewa kipaumbele na sisi wachungaji kabisa bali kama kweli tunataka hivyo vitu vya kifahari ni lazima tuwajhibike hata katika kazi ili tupate kwani ukwajibika ipasavyo Mungu hawezi kukuacha kamwe,” aliongeza.
Wakati huo huo alidai kuwa tabia hiyo imekuwa ikiwafanya hata baadhi ya watu wakose imani za kujaa na kupanda kwa kuwa wanaambiwa watoe na kisha watapata na badala yake hawapati bali ndio wanafilisika zaidi.
Alidai kuwa kwa kujiwekea utaratibu wa kujitukuza ovyo na kuwashusaha wale waliopo chini zaidi una madhara makubwa sana katika maisha ya kiroho lakini pia hata kimwili hivyo basi wale wote wanaofanya hivyo wanatakiwa kuacha mara moja.


No comments:

Post a Comment