Pages

Pages

Pages

Sunday 3 August 2014

MWANAJESHI WA ISRAEL ALIUAWA GAZA

Hodar Goldin mwanajeshi wa Israel aliyeuawa
Jeshi la Israel limesema kuwa mmoja wa wanajeshi wake ambaye aliaminika kutekwa na wapiganaji wa kipalestina ameuawa katika eneo la Gaza.
Jeshi la Israel limesema kuwa Hadar Goldin aliuawa wakati wa mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza.
Waziri mkuu nchni Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa Israel itaendeleza oparesheni zake katika eneo la Gaza hadi pale usalama wa raia wa Israel utakapoimarika.Israel ilikuwa imeishtumu Hamas kwa kumteka mwanajeshi huyo ,ambapo wapiganaji hao walikana madai hayo.
Hamas imesema kuwa itaendelea kupigana hadi pale itakapoafikia lengo lake.
Kundi hilo linataka kuhakikishiwa kuwa Israel na Misri zitafungua kizuizi cha mpakani cha miaka 7 kilichowekwa katka eneo la Gaza.
BBC

No comments:

Post a Comment