Pages

Pages

Pages

Monday 11 August 2014

KWA WADADA: UNATAKA TUMBO LAKO LIWE FLAT? FANYA HIVI - 7

LEO NI YOGA (Detox Yoga)
Urembo na mazoezi ni mambo yanayokwenda pamoja. Kama unataka kuongeza urembo wa umbile lako, hakikisha kwamba unakuwa muumini wa mazoezi na uzingatie vyakula vinavyofaa, hasa katika muendelezo huu wa mbinu za kulifanya tumbo lako liwe flat.
Leo ni siku ya saba ya mfululizo wa mazoezi au mbinu za mazoezi ya kuondoa unene wa tumbo na kwa hakika kama utayazingatia utakuwa na umbile bomba - kama lile ulilokuwa nalo kabla ya sasa au utaliboresha zaidi hili la sasa.
Katika mfululizo huo, leo tunazungumzia zoezi la Yoga - viungo. Kama mwili wako una mawasiliano mazuri, basi fanya mazoezi ya yoga na ufanye mazoezi haya katika hatua nane ambayo yatasaidia kila kiungo chako cha mwili kuwa fit.
Mazoezi haya yatasaidia sana kuimarisha mfumo wa mzunguko wa damu, mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, na mfumo wa mapafu kwa sababu utaondoa sumu nyingi mwilini, na mazoezi haya yatachochea mifumo hiyo kuwa bora zaidi.
Chagua ni hatua gani ya zoezi la yoga kati ya hizi na uifanye, lakini kama mwili wako una mawasiliano mazuri, basi unaweza kufanya mazoezi yote, na utakuwa katika safari ya kuwa 'mpya'. 








Kula salad
Hakikisha kwamba unakula salad yenye mchanganyiko wa matunda mbalimbali na usile chakula kinachoongeza mafuta na kujaza tumbo.

No comments:

Post a Comment