Pages

Pages

Pages

Monday 11 August 2014

KIMENUKA: SHIBUDA KUTOGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHADEMA 2015

Magare John Shibuda (kulia) akiwa na Rais Jakaya Kikwete

Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia Chadema, Magare John Shibuda, amesema kwamba hatagombea ubunge wa jimbo hilo kwa Chadema mwaka 2015.
Akizungumza na wazee wa jimbo hilo leo hii, Shibuda amesema tangu alipojiunga na chama hicho amekuwa akiandamwa kwa shutuma mbalimbali huku akitolea mfano tuhuma za hivi karibuni za yeye na wabunge wenzake Leticia Musobi Nyerere (Viti Maalum) na Said Arfi wa Mpanda, ambao wanadaiwa kuwa ni wasaliti kutokana na kitendo chao cha kushiriki vikao vya Bunge la Katiba wakati Ukawa wamelisusia.
"Mimi nimezingatia ushauri wa wazee kwamba mwaka 2015 nitafute chama kingine cha kuwatumikia, niachane na Chadema, kwa sababu tangu nimejiunga nacho nimekuwa sina amani, kila siku wananishutumu tu," alisema.

No comments:

Post a Comment