Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 1 July 2014

WATAKIWA KUTETEA PENSHENI KWA WAZEE BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot


ARUSHA: VIONGOZI wa kisiasa hapa nchini wametakiwa kuweka itikadi za  vyama vyao pembeni kuhusu Pensheni kwa wazee na badala yake  kwa pamoja wawe na sauti moja ya kuwatetea wazee wa nchi ya Tanzania.
Endapo kama kila mbunge bila kujali itikadi ya chama chake atafanya hivuo ni wazi kuwa ahadi ya pensheni kwa wazee itatimia na nchi itaweza kuokoa maisha yao kwa urahisi sana.
Kauli hiyo imetolewa na Javes Sauni ambaye ni mratibu wa jukwaa la wazee kwa mkoa wa Arusha (JUWA) wakati akiongea na wadau wa jukwaa hilo mapema jana kuhusiana na umuhimu wa pensheni kwa wazee wa Tanzania.
Sauni alisema kuwa umefika wakati wa Serikali kuweza kuona kuwa wazee wanahitaji kwa haraka Penseheni zao lakini ili Serikali iweze kuwasikia ni lazima kwanza viongozi wa siasa wawe  na umoja juu ya suala hilo.
Alisema kuwa suala la kuangalia maslahi ya wazee kama Pensheni haliitaji itikadi ya chama chochcote kile cha siasa bali linahitaji umoja madhubuti kwa viongozi hasa Wabunge na Mawaziri.
“Wawakilishi wa wazee hawa ndio hao wanatakiwa kukumbuka hata katika bajeti ya 2012/2013 Serikali ilidai kuwa italiangalia suala hilo lakini mpaka sasa bado halijatekelezwa sasa wao wanatakiwa kumuhoji Waziri mwenye dhamana hiyo na kama watafanya hivyo watakuwa wametetea maslahi ya wazee wengi sana," alisema Sauni.
Wakati huo huo aliongeza kuwa kutokana na wazee kukosa uangalizi wa kutosha pamoja na pensheni kama zilivyo nchi ambazo zimeendelea duniani kumesababisha changamoto kubwa kwa kundi hilo.
Alitaja changamoto hizo ni kama vile vifo vya aibu ambavyo vinatokea kila wilaya na kila Kata kwa kila saa moja ingawaje serikali bado ina ina uwezo mkubwa sana wa kuwasaidia wazee hao.
“Kama kundi hili la wazee litapata Pensheni ya uhakika basi litaweza kuondokana na vifo vya aibua ambavyo vinawakumba wazee hawa kwa kuwa wakati wanahitaji kitu kama vile dawa huwa wanakosa hivyo wanajikuta wanakufa kabla ya siku zao,kwaiyo kama wakiwa na pensheni wataweza kusaidia kuondokana na vifo hivi vya aibu”alifafanua hivyo.

No comments:

Post a Comment