Pages

Pages

Pages

Wednesday 2 July 2014

WAKATI NILIPOKUWA NA MAKAMANDA KATIKA MAKUMBUSHO YA FRELIMO, MATCHEDJE - MSUMBIJI

 Niko na 'makamanada' wa Jeshi la Msumbiji wakinizungusha katika Makumbusho ya FRELIMO. Mwenye kofia nyeupe ndiye walau anaweza kuzungumza Kiingereza na Kiswahili kwa mbali. Na mnara unaoonekana kwa nyuma umebeba majina ya makamanda wa jeshi la chama hicho walioshiriki kumng'oa Mreno. Hapo ndipo mahali ambapo Edwardo Chivambo Mondlane alihutubia mkutano wa pili wa chama hicho kuanzia Julai 20 – 25, 1968 baada ya ule wa kwanza wa Dar es Salaam na baada ya mkutano risasi zikaanza kupigwa dhidi ya Wareno. Hapa panaitwa Congresso, katika Wilaya ya Matchedje, Mkoa wa Niassa.
Getini pa kuingilia, makumbusho ya kihistoria haya, wakati nilipokwenda Congresso kujionea namna wenzetu walivyohifadhi historia yao.

No comments:

Post a Comment