Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 17 July 2014

VITA VYA GAZA KUSITISHWA KWA MUDA WA SAA TANO

Maombolezi,Mama wa moja wa watoto waliouliwa katika shambulio la Israel huko Gaza
Vuguvugu la kupigania Uhuru wa Palestina, Hamas, na Israel zimekubali kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza kwa muda wa saa tano baadaye hivi leo baada ya siku tano za mapigano makali.

Baada ya ombi la umoja wa mataifa jeshi la Israel limesema kuwa litasitisha mashambulizi kati ya saa nne asubuhi hadi saa tisa kwa saa za Gaza, ili kuwaruhusu wakaazi kupata chakula na huduma muhimu.
Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina Christopher Gunnes amesema kuwa ni matumaini yake kwamba usitishaji huo wa mapigano utatoa fursa ya kusuluhisha matatizo yanayoikabili gaza.Msemaji wa Hamas Sami Abu Zukhri amethibitisha kuwa vuguvugu hilo kadhalika litasitisha mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel wakati huo.
Makubaliano ya kusitisha vita ni ya mda, Hamas inadai hoja zao hazijatiliwa maanani
Hapo jana jumatano jazba zilizidi pale watoto wanne wa kipalestina wote kutoka familia moja waliuwawa katika shambulizi la mizinga kutoka Israel wakati wakicheza kwenye ufuo wa bahari huko Gaza.
Israel imesema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa Hamas na kwamba vifo hivyo ni matokeo ya mkasa mkubwa wa mapigano hayo.

Naye rais wa Marekani Barrack Obama amesisitiza kuwa Israel ina haki ya kujilinda.
(BBC)

No comments:

Post a Comment